Timu ya Mgambo JKT ya Tanga imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kutoa sare ya kufungana bao moja kwa moja na Wakata miwa wa Morogoro Mtibwa Sugar.
Mtibwa ambao walikuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao dakika ya 63 baada ya mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kuunganisha pasi na kufunga goli la kwanza.
Kipindi cha pili mpira ulikuwa wa kushambuliana na dakika ya 75 Mgambo waliandika bao kupitia shuti maridaki la Abuu Daudi na kumpita tobo kipa wa Mtibwa Said Mohammed.
Timu ya Mgambo ilistahili kupata ushindi hasa kwa vile ilicheza uwanja wa nyumbani lakini nafasi zake chache ilizopata ilishindwa kuzitumia.
Kocha wa Mtibwa, Mecky Mexine amesema pointi tatu kwao zinatosha kuwabakisha ligi kuu msimu ujao hivyo hana presha.
Kocha wa Mgambo JKT, Joseph Lazaro alisema kutoingia washabikiwa uwanjani kuishangilia kwake haoni tatizo kwani yeye ni kocha na timu ya watu wa Tanga hivyo kwake ni sawa tu.
Alisema timu hiyo iko mahututi hivyo ni miujiza ya Mungu tu kuibakisha ligi kuu msimu ujao.
No comments:
Post a Comment