Kamanda wa polisi Mkoani Tanga,
Leornard Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari magobore matatu na bastola moja
za kienyeji pamoja na vifaa vya kijeshi vilivyokamatwa Wilayani Kilindi wakati
wa msako wa kuwakata wahalifu na wanaojihusisha na ujambazi.
Jeshi la polisi Tanga limekuwa katika msako wa kuwatafuta wahalifu na majambazi ambapo hivi karibuni kumekuwa kukiripotiwa matukio mengi ya kihalifu ambapo juzi kamanda wa polisi Leonard Poul alisema amefanikiwa kuwauwa majambazi watatu katika mapango ya Mleni Ambini Mkoani humo na polisi wawili kujeruhiwa wakati wa mapambano.
No comments:
Post a Comment