Gari aina ya Semitrella lililokuwa na namba za usajili ya Kenya likiwa limegonga kingo za Daraja la Utofu Amboni Tanga barabara ya Tanga, Horohoro baada ya kufeli Breki na kukaribia kutumbukia mtoni ambao uko na Mamba wakali na mtu mmoja ambaye alikuwa abiria na kutojulikana jina lake alidondoka na kutumbukia mtoni. Jitihada za kutafutwa zilifua dafu baada ya mto huo kutoingilika kutokana na mamba wakali.
Daraja hilo ambalo liko na urefu zaidi ya mita 200 liko na mteremko mkali wa mlima na baadhi ya mashuhuda wa ajali hilo walidai kuwa waliliona gari hilo likiserereka na kukosa mwelekeo baada ya breki zake kufeli.
No comments:
Post a Comment