Besigye akamatwa kwa 'kujiapisha' Uganda
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.
Video hiyo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
Mgombea huyo wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Forum for democratic change FDC- alikamatwa na polisi kwa'' kukaidi amri halali''.
Matukio hayo yanawadia wakati ambao viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na wageni mashuhuri wameanza kuwasili mjini Kampala ilikuhudhuria kuapishwa kwa rais Museveni hapo kesho.
Tangu matokeo ya uchaguzi kutangazwa mwezi Februari, Dr Kiiza Besigye amekuwa chini ya ulinzi mkali nyumbani kwake baada ya kupinga matokeo yaliyompa rais Museveni ushindi.
No comments:
Post a Comment