Dar es
Salaam. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umelitaka Bunge
kuiwajibisha Serikali ikiwa Rais Jakaya Kikwete atashindwa kutekeleza
maazimio ya Bunge ikiwamo kumng'oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo.
Wakizungumza
hapa jana, viongozi hao walisema endapo Rais atashindwa kumwajibisha
Profesa Muhongo, basi wabunge wao watawasilisha hoja na kushawishi
wengine kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na umoja huo
utaitisha maandamano nchi nzima.
Mwenyekiti
mwenza wa umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba alihoji kwa nini Rais
Kikwete anasita kumwondoa Profesa Muhongo wakati Bunge lilishatoa
maazimio.
Alisema
Bunge linalowakilisha wananchi zaidi ya milioni 45 liliazimia uteuzi huo
utenguliwe lakini akaelezea kushangazwa kwake na hatua ya Rais kusema
bado anachunguza.CHANZO:MWANANCHI
"Hivi
Rais anachunguza nini, haliamini bunge? Kama anavyoteua mawaziri pia ana
madaraka ya kutengua nafasi zao, sasa anasita nini wakati azimio la
Bunge limemwelekeza. Kama Rais Kikwete atashindwa kumwajibisha Muhongo
atakuwa ameshindwa kutekeleza moja ya maazimio ya Bunge na Ukawa
utaliomba Bunge kuiwajibisha Serikali."
Alisema
hotuba aliyoitoa Jumatatu wakati akiwahutubia wazee wa Mkoa wa Dar es
Salaam, haijakidhi matarajio ya wengi kwani kuna maazimio
hayajatekelezwa.
Profesa
Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, alisema Rais amekataa
kutekeleza azimio la kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe na kutoa sababu
ambazo hazina mashiko.
"Tangu
mitambo ya IPTL imefungwa Taifa limepata hasara kubwa kwa sababu umeme
unaouzwa ni wa gharama kubwa kuliko mitambo yoyote ya umeme inayotumika
katika bara la Afrika, Taifa limeingia hasara kubwa, Rais aitaifishe,"
alisema Profesa Lipumba.
Alisema
katika hotuba hiyo Rais Kikwete alionyesha kuipendelea IPTL na
kuikandamiza Tanesco wakati akielezea kuwa fedha za escrow zilikuwa mali
ya IPTL.
Alitaka
hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika na ufisadi wa
Akaunti ya Tegeta Escrow na wengine walionufaika nazo.
"Sheria ya maadili itungwe upya ili iweke uwazi wa mtu yeyote kuona taarifa ya mali za viongozi."
Mbatia na Dk Slaa
Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia aliwataka viongozi wa dini kuliombea
Taifa katika kipindi hiki ambacho mihimili ya dola inapingana.
"Tuna
matatizo makubwa, malori ya fedha yanachotwa benki kwa siku moja lakini
Usalama wa Taifa hawashtuki, viongozi wa dini liombeeni Taifa, tuna
mtikisiko," alisema Mbatia.
Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema amesikitishwa na hotuba ya
Rais kwa kutowataja wahusika waliochota Sh73 bilioni katika Benki ya
Stanbic wakati kuna Idara ya Usalama wa Taifa.
"Hivi kweli Serikali yenye Usalama wa Taifa haiwafahamu waliochota fedha hizo?" alihoji Dk Slaa.
LHRC yashangazwa
Wakati
viongozi hao wakisema hayo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
kimeeleza kusikitishwa kwake na utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge
juu ya sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mkurugenzi
Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo - Bisimba alisema katika taarifa yake
kuwa hotuba ya Rais Kikwete kupitia kwa wazee wa Dar es Salaam Jumatatu
iliyopita, iliikumbatia kampuni ya IPTL na kutupa maazimio mengi ya
Bunge kutokana na kutochukuliwa hatua zilizotarajiwa.
Licha ya
kwamba tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema
ameshajiuzulu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa
Anna Tibaijuka, kufutwa kazi na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini,
Eliakimu Maswi kusimamishwa kazi, Dk Bisimba alisema Rais hakuchukulia
suala hilo kwa uzito na kwa kiwango kinachotakiwa.
Alisema
badala yake, hotuba ya Rais ilijaa masihara katika kashfa nzito inayoipa
kibarua kigumu Serikali katika kupambana na rushwa.
Alimtaka
Rais Kikwete apokee heshima aliyopewa na Bunge ya kufanya uamuzi na
kwamba kutofanya hivyo kutamshushia heshima kwa Watanzania.
Dk
Bisimba alisema masuala ya escrow, umiliki wa PAP/IPTL, tuhuma za rushwa
na kodi za Serikali yalikuwa yameshafafanuliwa na Kamati ya Bunge na
Hesabu za Serikali (PAC) lakini kwa bahati mbaya, Rais aliyarudia upya
na kuegemea upande wa IPTL.
"Rais
katika hotuba yake alikuwa anapangua kila hoja kiasi kwamba alitoa
hitimisho la kuwa fedha zilizokuwa kwenye akaunti ile hazikuwa za
Serikali, bali za IPTL, jambo ambalo si sahihi."
Alisema
kauli ya kutaka uchunguzi uendelee juu ya masuala hayo inaibua utata wa
uchunguzi ufanywe na nani tena zaidi ya Bunge kupitia CAG na Takukuru na
kwamba matokeo yake apewe nani?
Mdee: Tibaijuka abanwe zaidi
Waziri
Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee alisema Rais
Kikwete anatakiwa kumchukulia hatua zaidi Profesa Tibaijuka ili iwe
fundisho kwa watumishi wengine wa umma.
Kauli
hiyo ya Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema) inatokana tuhuma za
ukosefu wa maadili kwa waziri huyo baada ya akaunti yake binafsi
kuingiziwa Sh1.6 bilioni katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow,
ambazo alisema zilikuwa za kusaidia shule.
Akizungumza na gazeti hili jana Mdee alisema: "Suala hili halitakiwi kuishia kwa kumvua uwaziri.
Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu anatakiwa kuchukua hatua zaidi ya hapo ili kuwa fundisho wa watumishi wengine.
"Rais
Kikwete ndiye anayeweza kuifanya nchi hii ikaendelea zaidi na yeye
mwenyewe anaweza kuwafanya viongozi wake wakawa wawajibikaji na
waadilifu lakini ukisema mtu anakosea unamfukuza kazi, tutakuwa
tunafanya mambo ya kuigiza. Rais azingatie ipasavyo maazimio ya Bunge
kama yanavyosema."
Alipoulizwa
atamkumbuka kwa lipi waziri Profesa Tibaijuka katika wizara hiyo, Mdee
alisema, "Katika kipindi chote akiwa waziri wa ardhi sina cha kumkumbuka
kwani migogoro ya ardhi ndiyo kwanza imeongezeka, wakulima na wafugaji
kila kukicha ni mapigano, tunahitaji mtu atakayeiongoza wizara hiyo
ipasavyo na kupunguza migogoro ya ardhi inayogharimu uhai wa wananchi."
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment