Friday, December 5, 2014

Adakwa akiwa na misokoto 7 ya bangi



Kumekucha blog

Tanga, JESHI la Polisi kituo kikuu cha Chumbageni Tanga, kinamshikilia Said Khamis (28) mkazi wa Pongwe  kwa tuhuma za kupatikana na kilo 1  na misokoto 7 ya bangi wakati wa msako wa safishasafisha wauzaji na walaji wa madawa ya kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kaimu kamanda wa polisi Mkoa, Juma Ndaki, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa 5 asubuhi baada ya jaribio lake la kuwatoroka polisi kushindikana.
Alisema polisi iko katika msako wa kuwatokomeza watumiaji na wauzaji wa madawa ya kulevya na kuwafikisha mahakamani lengo likiwa ni kutokomeza magenge ya uvutaji na uuzaji wa madawa hayo.
“Unajua kuwa kipindi hiki ni cha harakati nyingi zikiwemo za kuelekea sikukuu ya krismas na mwaka mpya----polisi inalazimika kuweka mazingira mazuri ya wananchi kusherehekea” alisema Ndaki
“Polisi imezidisha doria usiku na mchana na hata ninyi waandishi wa habari nadhani huko mitaani kwenu munawaona vijana wetu wakipita----ila niwaambie wananchi wasitishike wakiona askari wako na mbwa na mabunduki begani” alisema Ndaki
Akizungumzia hali ya uhalifu, Ndaki alisema polisi wameweza kuzima matukio ya uporaji wa kutumia nguvu nyakati za usiku ukiwemo wa pikipiki na baskeli pamoja kuharibu mitambo ya utengenezaji wa pombe aina ya gongo.
Alisema jumla ya mitambo mitano katika maeneo tofauti walitekeleza na kuiharibu na wamiliki kufikishwa mahakamani  jambo ambalo limesaidia kuwepo kwa hali ya usalama mitaani.
Alisema magenge hayo ya unywaji wa pombe imekuwa ikizalisha magenge ya kihalifu  na kusababisha wazazi kuongozana na watoto wao wadogo katika vilabu na kuwa chanzo cha kuacha masomo shuleni.
“Jumla ya mitambo mitano ya utengenezaji wa pombe aina ya moshi imetekelezwa na kuharibiwa katika kipindi hiki cha safishasafisha utumiaji wa madawa ya kulevya na wauzaji” alisema Ndaki
Akitoa wito kwa wananchi kaimu huyo kamanda, aliwataka kutoa taarifa kwa jeshi hilo wanapona matukio pamoja na watu ambao hawatambuliki wakijihusisha na vitendo vinavyohusiana na uhalifu.
 Kumekucha blog

No comments:

Post a Comment