Hekaheka inahusu mwanaume aliyepotea mazingira ya utata baada ya kufunga ndoa Tanga
Bwana huyo amesema siku ya Jumapili
alikwenda nyumbani kwa wakwe zake kuaga lakini akiwa njini kurudi
alikutana na msichana mdogo akitokea mbele yake lakini kadri walivyokuwa
wakikaribiana msichana huyo alizidi kuwa mrefu, akataka kugeuka
kukimbia ambapo akakuta kuna watu wengine wawili nyuma yake ambao
walimwagia maji akapoteza fahamu.
Baada ya kuzinduka alijikuta amewekwa
sehemu huku waliomzunguka wakijadiliana kumkata ulimi na wengine
wakipingana na mawazo hayo, baadaye walimpeleka kwenye mti na
kumlazimisha ale nyama ambayo hakujua ni nyama ya nini kisha wakampeleka
baharini ambako kulikuwa kumewekwa sherehe nako walitaka kumkata ulimi
pia akakataa ambapo kati ya watu hao wapo waliokuwa wakikataa pia
kumkata ulimi.
Alifanikiwa kuwasiliana na ndugu zake
kwa njia ya message mpaka wakafika mahali ambapo watu hao walimuacha,
anasema kwamba anawatambua watu wote waliokuwa wakimfanyia mauzauza hayo
japo amegoma kuwataja kwa mke wake.
No comments:
Post a Comment