POLISI WAWILI WAUWAWA NEW YORK
Gari la polisi waliokuwemo polisi wawili waliouwawa mapema leo Brooklyn New York.
Na Mwandishi wa Vijimambo, New York
Polisi
wawili wameuwawa mjini Brooklyn New Yrk na mtu ambaye inasemekana
amesafiri toka Baltimore Maryland kwa kukusudia kufanya mauaji hayo na
baadae kujipiga risasi baada ya kuzingirwa na polisi ndani ya kituo cha
treni.
Polisi
wawili waliouwawa Wenjan Liu na Rafael Ramos waliuwawa siku ya jumamosi
mchana Desemba 20, 2014 wakiwa ndani ya gari lao wakiwa wameegesha mjini
Brooklyn, New York wakiwa katika zamu yao ya kula lindo kwenye kazi yao
ua upolisi.
Muuwaji
huyo Ismaaiyl Brinsley miaka 28 aliwauwa polisi hao kwa kuwafyatulia
risasi vichwani na sehemu ya mwili juu kifuani kupitia dirisha la abiria
ya gari hiyo ya polisi iliyokua imeegeshwa kati ya mtaa wa Martle na
Tompkins na polisi hao kufa papo hapo kwenye eneo la tukio huku muuaji
akijipiga risasi na kufa baada ya kuzingirwa na polisi na baada ya kuona
hakuwa na pakutokea.
Bwn.
Brinsley inasemekana kusafiri kwake kuja kufanya mauaji hayo ya polisi
ni kutokana na kutopatikana na kosa kwa polisi waliosababisha kifo na
mmarekani mweusi Eric Garner aliyekabwa
koo na polisi waliokwenda kumkamata na baadae kupoteza maisha kwenye
eneo la tukio japo mtuhumiwa huyo alikuwa akiwaambia polisi hao hawezi
kupumua na polisi waliendelea kumkaba koo mpaka akapoteza maisha jambo
lililowaudhi wamarekani weusi wengi akiwemo muuwaji wa polisi hao
alifanya mauaji hayo kwa kukusudia kulipiza kisasi kwani alinukuliwa na
vyombo vya habari akisema atakwenda Brooklyn New York kwa adhma ya
kutekeleza nia yake hiyo.
No comments:
Post a Comment