HADITHI
KISIWA
CHA HARISHI (8)
ILIPOISHIA
TOLEO LILILOPITA
Mara
kwa mara nilikuwa nikitupa macho kila upande wa chumba hicho kwa hisia kwamba
Harishi angeweza kutokea mle chumbani.
Asubuhi
kulipokucha Yasmin alikuja kutugongea mlango.
“Amkeni.
Kumeshakucha” Alikuwa akituambia wakati akigonga. Tukatambua kuwa alikuwa ni
yeye.
Tukafungua
mlango.
“Mmeamkaje?”
akatuuliza.
“Tunashukuru
tumeamka salama” nilimjibu kwa niaba ya wenzangu.
Wenzetu
waliolala chumba kingine walikuwa hawana habari ya tukio lililotokea usiku.
Nikawaeleza mbele ya Yasmin. Wakasikitika sana
na kupata hofu.
“Sasa
nendeni mkaoge halafu niwaandalie chai” Yasmin akatuambia.
Tukaenda
kuoga. Kwanza waliingia watu wanne kwa vile
vyoo vilikuwa vine. Walipotoka nikaingia mimi na mwenzangu.
Yasmin
akatuandalia chai pale sebuleni. Ilikuwa chai iliyotengezwa kwa maziwa ya unga
na iliyoungwa kwa iliki, tangawizi na bdalasini. Pia alitupa mikate
iliyotengezwa kwa mayai.
SASA ENDELEA
Yeye mwenyewe alikunywa chai
pamoja na sisi. Nikamuona amefurahi na kuchangamka licha ya kwamba usiku wa
jana yake tu tulishuhudia machungu ya kuuawa mwenzetu.
“Ningekuwa nakula na wageni
kila siku namna hii ningechangamka, lakini mh!” Yasmin alisema kama aliyekuwa akisema pek yake.
“Ni kweli Yasmin lakini
tutafanyaje? Tunapenda kukusaidia lakini hatuna uwezo. Kama
hivyo umeona mwenzetu ameshauawa na sisi hatujui maish yetu yatakuwaje!”
nikamwambia Yasmin kwa huzuni.
“Kusema ukweli napenda
niendelee kuwa na nyinyi hapaili nipate wenzangu wa kuzungumza nao. Lakini
haitawezekana nyinyi muwepo hapa mkiwa hai.”
“Na pia hatuna mahali pengine
pa kwenda” nikamwambia Yasmin.
“Huu ni mtihani. Sijui
mtatumia mbinu gani muwe salama”
“Labda tuendelee
kujifichaficha humu ndani” Mwenzetu mmoja akaingilia yale mazungumzo.
“Humu ndani atawagundua tu”
Yasmin akamjibu.
“Sasa tutakwenda wapi
jamani!”
“Mimi sijui niwambie nini
ndugu zangu!” Yasmin akatuambai.
Tulipomaliza kunywa chai
Yasmin aliondoa vyombo. Alituacha tumekaa tukiendelea kujadiliana. Baadaye
kidogo alirudi akiwa na karata.
“Hizi karata ziko siku zote.
Huyu mwendawazimu ananiletea. Lakini sina mwenzangu wa kucheza naye”
Tulipoona karata tukazunguka
duara. Yasmin akakaa na kutugawia.
“Tunacheza mchezo gani?” nikamuuliza
Yasmin.
“Tunacheza mchezo wa
arbasitini”
Mchezo huo ulikywa maarufu
kule Zanzibara na Comoro.
Tukaanza kucheza karata.
Tukasahau kabisa habari ya Harishi. Mchezo ulinoga sana. Kelele zetu zikawa zinasikika hadi nje.
Ilipofika saa tano Yasmin akavunja
mchezo na kutuambia tukatembee tembee. Tukiona jua la saa saba ndio turudi kula
chakula. Mda ule alitaka kwenda kupika chakula.
“Niwapikie nini?” akatuuliza.
“Tupikiechochote tu
utakachopenda” nikamwambia.
“Basi nitawapikia pilau”
“Tutashukuru sana”
“Sasa mtakapokuja, kwanza
mchungulie na kusikiliza. Mkimuona Harishi msiingie ndani, rudini huko huko
mtakakotoka. Anaweza kuja ghafla”
“Tumekuelewa” nilimjibu.
Baada ya hapo tulitoka
tukarudi kule kwenye boti letu.
Ni tabia ya maumbile ya
binaadamu kutokata tama na kujaribu kubahatisha kila mara hasa kwa watu
kama sisi ambao tulikuwa katika hatari. Kwa mara nyingine
tulijaribu tena kuliwasha lile boti. Kila mmoja wetu alijaribu kuliwasha
bila
mafanikio.
Tukakaa chini ya mti na
kuanza kujadiliana. Hata hivyo mjadala wetu ulikuwa kama
usio na maana yoyote kwani haukutupa ufumbuzi wa jinsi ya kusalimisha maisha
yetu.
Kikubwa tulichokizingatia ni
kujaribu kumkwepa Harish kadiri itakavyowezekana. Tuliona kama tutafanikiwa
kumkwepa tunaweza kuendelea kuishi.
Tuliendelea kukaa pale chini
ya mti hadi saa saba tulipoamua kurudi kwa Yasmin. Tulimtuma mmoja wetu aingie
akachunguze kama Harishi yuko ndani aje
atuambie.
Mwenzetu huyo akaingia ndani.
Sisi tukawa tunamchungulia kwenye dirisha. Alinyata hadi ndani. Tukawa
hatumuoni tena. Tukahamia kwenye dirisha jingine. Tukamuona amesimama pembeni
mwa ukumbi akiangalia huku na huku. Akaenda jikoni kuchungulia kisha akatoka.
Alipotoka jikoni alikwenda
moja kwa moja kwenye mlango wa chumba cha Yasmin na kutega masikio yake kwenye
mlango. Alisikiliza kwa muda kidogo kisha akaanza kugonga mlango taratibu.
Mlango ukafunguliwa ghafla.
Aliyetoka alikuwa Yasmin. Alitoka haraka haraka akaufunga mlango kisha
akamuashiria yule jamaa aondoke. Nikajua kuwa hapakuwa salama.
“Moshi unajaa kwenye chupa,
Harishi anakuja!” Yasmin alimwambia.
Yule mwenzetu aliposikia vile
aligeuka ili aondoke lakini ghafla tena mlango ukafunguliwa. Harish akaibuka
mbele ya yule mtu. Alikuwa ameshika upanga wake. Akamshika yule jamaa kwa mkono
mmoja.
“Unataka ukimbie wapi wewe?”
akamuuliza akiwa amemtolea macho.
ITAENDELEA KESHO
USIPITWE NA KISA HIKI CHA KUSISIMUA KESHO NI KITATOKEA
No comments:
Post a Comment