Umekuwa busy na kushindwa kusoma Magazeti ya leo December 13? Hapa nimekuchambulia Story kubwa tano
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam ameagiza
Halmashauri ya Jiji kuziondoa haraka kampuni zote za udalali
zinazokamata magari yanayovunja Sheria za maegesho baada ya kupongezeka
malalamiko ya vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na kampuni hizo.
Baadhiya Kampuni ambazo zimetajwa ni
Yono Auction Mart & Co Ltd, Tambaza Auction Mart & General Court
of the Tribunal na Mwamkinga Auction Mart.
Baadhi ya kero zilizotajwa ni pamoja na
kukamata magari yaliyopaki kwenye nyumba za watu, wamiliki wa magari
kulazimishwa magari yao kuvutwa wakati yana uwezo wa kutembea yenyewe,
kufukuzwa magari kwa madai kuwa yameegeshwa vibaya na pamoja na kutozwa
faini kubwa tofauti na kiwango kilichowekwa kisheria.
Sadiki amezishauri Halmashauri za Dar kuingia mkataba na Kampuni ya Ulinzi na Usalama ya Suma JKT.
MWANANCHI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na
Teknolojia, John Mngondo amesema Nchi za Afrika bado zinakabiliwa na
changamoto kubwa ya wakazi wengi kutokuwa na anuani za makazi ambapo
hiyo inatajwa kama moja ya sababu zinazopelekea kucheleweshwa kwa
maendeleo.
Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo katika
Mkutano wa siku tatu uliowashirikisha wadau wa Posta ulioandaliwa nan a
Umoja wa Posta Afrika (PAPU) pamoja na wadau wengine, huku akiakiongeza
kuwa changamoto hiyo iunachangiwa na miuondombinu mibovu.
MTANZANIA
Umoja wa waendesha Bodaboda na Bajaj Dar
es Salaam wamesema wanampa Rais Kikwete siku 14 kushughulikia maombi
yao ya kuruhusiwa kusafirisha abiria katikati ya Jiji kinyume na hapo
wataitisha maandamano ya amani kushinikiza ombi lao kutekelezwa.
Mwenyekiti wa Chama hicho Said Chenja
amesema hawaridhishwi na namna ambayo watendaji wa chini wa Rais
wanavyoshughulikia suala hilo.
Mwenyekiti huyo amesema suala la utoaji
wa vibali maalum limekuwa likiufabywa kwa upendele mkubwa huku vibali
hivo vikiwa na mapungufu ya kutokuwa na maelekezo ya maeneo ambayo wale
waliopewa vibali hivyo wanaruhusiwa kuingia na ambako hawaruhusiwi.
JAMBO LEO
Kiwanda cha kuzalisha Sukari cha
Kilombero kiko hatarini kufungwa kutokana na kukosekana kwa soko la
Sukari inayozalishwa kiwandani hapo ambapo jumla ya ajira 75,000
zitaathiriwa na hilo na zaidi ya wakulima zaidi ya 15,000 wanaolima zao
hilo pia kujikuta wakipoteza vyanzo vya mapato.
Wakulima na wafanyakazi hao wameiomba
Serikali kuangalia namna ya kuisuru hali hiyo huku kwani maisha yao
yanategemea kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
Changamoto ya uingizwaji wa Sukari kutoka nje bila kutoza ushuru imeathiri sehemu kubwa ya soko la bidhaa hiyo ndani ya nchi.
NIPASHE
Mama mmoja mjamzito, Grace Frederick na
mtoto wake Braiton Said mwenye umri wa miezi 11 walikamatwa na Polisi
Chato, December 07 mwaka huu baada ya kudaiwa kumfungia wifi yake,
Mwanvua Said ambaye inasemekana alitaka kuhamisha vitu bila taarifa ya
mume wake.
Grace aliwekwa ndani na mtoto wake ambaye anasema wakati wa usiku alilia sana kutokana na kushikwa na njaa.
Hii ni kinyume na ambavyo inatakiwa
kufanyika kwani Serikali na Mashirika mbalimbali wamekuwa wakiendesha
kampeni za kupunguza vifo vya Wanawake wajawazito na watoto chini ya
mwaka mmoja.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, Alex Musama alisema kuwa hajapata taarifa zozote kuhusu madai hayo.
Unahitaji kupata story zote kali zinazonifikia? Ni rahisi sana mtu wangu.. Niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment