TANGA KUMEKUCHA

Thursday, December 18, 2014

KISIWA CHA HARISHI

HDITHI HII INALETWA KWENU KWA HISANI YA MKOMBOZI SANITARIUM CLINC,TANGA WALIOKO CHUDA , TANGA
KISIWA CHA HARISHI
 
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
 
“Unahakika kuwa nitakuwa salama?”
 
“Harishi hatakuja leo. Ameshakuja asubuhi ni mpaka kesho”
 
“Ngoja niwaage wenzangu”
 
Tukatoka ukumbini. Wenzangu walikuwa wameketi wakizungumza. Nikawambia kwa namsindikiza Yasmin.
 
“Ninakwenda kupika, nitampa chakula awaletee” Yasmin akawambia.
 
“Yaani utasubiri chakula huko huko?” Mmoja akaniuliza lakini uso wake haukuonesha furaha.
 
“Ndio atakisubiri” Yasmin akamjibu.
 
Masudi akawatazama wenzake kabla ya kuniambia.
 
“Sawa. Sisi tutasubiri”
 
Jina lake lilikuwa Masudi. Katika sisi watu wanne tuliobaki, yeye alikuwa ndiye mkubwa kwetu kiumri.
 
SASA ENDELEA
 
Wakati mimi na Yasmin tunatoka kwenye ile nyumba tukirudi nyumbani kwa Yasmin, Yasmin aliniambia. “Yule kaka uliyezungumza naye anaitwa nani?’
 
“Anaitwa Masudi”
 
“Naona kama hakufurahi ulivyomwambia tunatoka mimi na wewe”
 
“Inawezekana, ni binaadamu. Labda ameona tumewabagua”
 
“Mbona wengine hawakusema kitu?”
 
“Kila mtu ana mawazo yake. Yule amezoea kutuamrisha kwa sababu kwenye kundi letu yeye ndiye mkubwa kiumri na amekuwa kama kiongozi wetu”
 
“Kwa hiyo alitaka anisindikize yeye”
 
Yasmin aliposema hivyo nilicheka, na yeye akacheka.
 
“Unafikiri nakutania?” aliponiuliza hivyo alitaja jina langu.
 
“Hunitanii, unaniambia ukweli. Najua Masudi hakufurahi” nikamwambia.
 
Pakapita kimya kifupi kabla ya Yasmin kuniambia.
 
“Kisiwa chote hilki kilikuwa kina watu”
 
“Wewe uliwakuta hao watu?” nikamuuliza.
 
“Wakati Harishi ananileta hapa alikuwa ameshamaliza watu wote. Wengine walihama wenyewe kukimbia kifo”
 
“Na kama leo anakuja na kutukuta hivi itakuwaje?”
 
“Atakukamata wewe. Atakufyonza damu na ndio ataniuliza wewe ni nani na ulifuata nini hapa”
 
“Ina maana wewe hatakuadhibu?”
 
“Ananitisha tu pale ninapomuudhi lakini kama atanikuta na mwanaume nadhani ataniadhibu”
 
“Lakini hatakufyonza damu?”
 
“Hapo siwezi kujua”
 
“Inatisha. Ni kwa vile tu umenihakikishia kwamba hatarudi tena leo”
 
Tulipofika katika jumba la Yasmin. Tulikaa katika ule ukumbi tukaanza kuzungumza.
 
Yasmin akanieleza wazi kuwa alikuwa amenipenda.
 
“Wewe ndio ungefaa uwe mume wangu” akaniambia kiudhati.
 
“Tayari umeshakuwa mke wa jini, huwezi tena kuwa mke wangu”
 
“Jini amenioa wapi? Si ananibaka tu!”
 
“Lakini ndio mume wako na amekuleta huku kusudi aweze kukudhibiti”
 
“Hakuna kisichokuwa na mwisho. Mwisho wake utafika tu”
 
“Inshaallah!”
 
“Mimi na wewe tutakwenda kuoana Comoro!”
 
Nikatikisa kichwa changu. Niliona Yasmin alikuwa anaota ndoto ya mchana.
 
“Yasmin huoni kuwa tuko jela! Unawazia kwenda kuoana Comoro, hapa tutatoka vipi?”
 
“Tutatoka tu iko siku. Kila siku mimi naswali kuomba”
 
“Angekuwa ni mwanaadamu aliyekuweka hapa tungepambana naye. Lakini jini aliyemaliza kisiwa kizima ni hatari”
 
“Usikate tama, usinivunje moyo. Wewe mwanaume!” Yasmin aliposema hivyo alinyanyuka.
 
“Ngoja nikapike sasa” akaniambia na kuelekea jikoni.
 
Wakati anatembea nilimtazama kwa nyuma. Nguo alizokuwa amevaa zilimpendeza. Kama alivyotueleza mwenyewe nguo hizo alikuwa naletewa na Harishi ambaye huziiba kwnye maduka ya miji mikuwa.
 
Yasmin alipofika kwenye mlango wa kuingilia ndani aligeuka na kunitazama. Alipoona nilikuwa namuangalia akatabasamu kabla ya kuingia ndani.
 
Nilikaa peke yangu nikiwaza hili na lile. Nilijiambia Yasmin alikuwa msichana mzuri, kikwazo kilikuwa ni lile jini. Kama nafanikiwa kumuoa binti wa rais ni heshima kubwa.
 
Baada ya muda kidogo niliondoka nikamfuata Yasmin jikoni.
 
“Umenifuata huku?” Yasmin akaniambia.
 
“Nataka tusaidiane kupika” nikamwambia kwa mzaha.
 
“Si ungekaa tu nikakupikia mume wangu mtarajiwa”
 
Nilijua Yasmin alikuwa anajifariji kuniita “mume wangu mtarajiwa” Na mimi sikutaka kumvunja moyo. Kwa upande mwingine mimi pia nilihitaji faraja kutoka kwa Yasmin.
 
“Hapana nataka nikusaidie mtarajiwa wangu”
 
“Haya nisaidie”
 
Nikamsaidia Yasmin kupika huku mizaha na dhihaka zikipita. Kwa mara ya kwanza niligundua Yasmin alikuwa mchangamfu na aliyependa mzaha. Alikuwa akicheka hadi sauti yake ilisikika nje. Alikuwa amesahau kabisa mateso yaliyokuwa yanatukabili sisina yeye.
 
“Yasmin unacheka sana, sauti yako inasikika nje”  nikamwambia.
 
“Kwani nani atatusikia, si tuko peke yetu?”
 
“Najua tukompeke yetu lakini usicheke sana”
 
 
ITAENDELEA KESHO








Imechapishwa na Unknown kwa 9:46 PM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Time

 Time in Tanga

Total Pageviews

My Blog List

Blog Archive

  • ▼  2014 (563)
    • ►  November (97)
    • ▼  December (466)
      • MTOTO WA GWIJI WA KONFUU CHINA ASWEKA JELA BAADA ...
      • POLISI WATOA TAHADHARI SIKU ZOTE ZA SIKUKUU ZA KRI...
      • MTOTO WA MIAKA SITA AMUOMBA OBAMA AFANANE NAE
      • KOLOBO YA AY NA KINGSTONE NDANI YA LUNINGA
      • ESCROW YAFYEKA MWENGINE,NI ELIAKIM MASWI
      • DIAMOND PLATNUMZ NDANI YA MJENGO NA JK
      • MASIKINI, MAJAMBAZI BILA KUMKUSUDIA WAMEMPIGA RISA...
      • AMKA ZA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG
      • DIAMOND MACHO KODOKODO, HANA UTULIVU
      • KISIWA HARISHI SEHEMU YA (17)
      • POLISI TANGA YACHARUKA
      • MSICHANA ALIEMTUPA MTOTO CHOONI KUMBE ANA LAKE
      • CAROLYNE BERNARD ASHINDWA KUJITOKEZA
      • NDIE KWELI HUYU TIBAIJUKA TUNAYEMFAHAMU JAMANI ?
      • D 'BANJ ATOKA KIAINA
      • MAAAJABU, MOVE YA KIMAREKANI KUTENGENEZWA DAR , BI...
      • TID, ASEMA NENO
      • MVUA YA MAWE YASOMBA NYUMBA MIA MBILI, SINGIDA
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG
      • WATOTO 11 WAZALIWA BOMBO MKESHA WA KRISMASS
      • WATOTO 11 WAZALIWA MKESHA WA KRISMASS BOMBO
      • SOMA MKUSANYIKO WA STORI ZA MAGAZITI YA LEO,TZ
      • WAHANGA WA AJALI YA MELI WAZIKWA,KONGO
      • AJALI, MWENDO KASI
      • FAMILIA YALAZIMIKA KUHAMISHIA MAKAZI NJE YA NYUMBA
      • Jamii yatakiwa kuwapa malezi bora watoto wao
      • MISS TANZANIA 2014 ABWAGA MANYANGA
      • UKAWA WACHACHAMAA NA ESCROWS
      • ILI UWE MWANACHAMA WA AZAM FC, LAZIMA UWE NA KADI
      • KUMRADHIIIIIIIIIIIIIIIIIII
      • TAMASHA TUONANE JANUARY LAFANA MORO,SI MCHEZO HEBU...
      • MUSSA CHITEPETE APATIWA VIFAA VYA MASUMBWI
      • MWANA MPOTEVU KUREJEA NYUMBANI
      • VITUKO VYA MASTAA
      • VIJANA WATATU MBARONI KUTAKA KUIBA SANAMU YA BIKIR...
      • FURAHA YA SIKUKUUU, RASKAZONE TANGA JANA
      • KISIWA HARISHI
      • MAAJABU, WANAUME NAO KUNYONYESHA?
      • VICHWA VIKUU VILIVYOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO TZ
      • AUWAWA KWA KILE KINACHODHANIWA KURIPUKIWA NA BOMU,...
      • DUNIA IMEKWISHA,STARA AIBU IMEPOTEA
      • NHC KUWAPELEKA WATOTO 53 WENYE MARADHI YA MOYO INDIA
      • CHALSEA MWENDO MDUNDO
      • SIMBA BADO KAZI NENE
      • POLISI SONGEA INAWASAKA WATU WATATU KWA KUJIHUSISH...
      • MAN MWENDO MDUNDO
      • CHEKI TIMU YAKO IKO KATIKA NAFASI YANGAPO
      • ARSENAL YAZINDUKA, YASGINSA 2, 1
      • AMKA ZA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG
      • KISIWA HARISHI (19)
      • JE ,SIKU YA LEO NAWE UTAPATA ZAWADI?
      • SOMA STORI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO NA MAGAZETI YA L...
      • WAFUKUZWA KAZI MATUMIZI MABAYA YA SIMU, CHINA
      • KOREA KASKAZINI YAIKOMALIA MAREKANI, YALETA KEBEHI
      • CHRIS BROWN NA KARRUECHE WAWEKA TOFAUTI ZAO KANDO,...
      • WEMA ,ANTI EZEKILE WAWA GUMZO MITANDAONI
      • NDOA YAVUNJIKA ,KISA KIJUBADILISHA AFANANE NA KIM ...
      • AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG
      • KISIWA HARISHI (20)
      • WAHAMIAJI HARAMU SITA WANASWA, MUHEZA TANGA
      • BIASHARA , USAFI
      • NDEGE YA ABIRIA YAPOTEA WATU 160 WAHOFIWA KUPOTEA
      • DIAMOND KAMA MFALME UGANDA
      • MWAKYEMBE ACHOCHEA MOTO WA SUMATRA
      • AMUUWA MKE WAKE KWA SHOKA KUMKOSEA KITOWEA CHA KU...
      • 50 CENT AVUNJA UKIMNYA MAUAJI YA WAMEREKANI WEUSI
      • YANGA, AZAM NGOMA NDROOO
      • MATOKEO MAZIMA YA YANGA NA AZZAM HAYA HAPA
      • ATUMIA MBINU MBADALA KUMREJESHA MPENZI WAKE
      • WENGER AUNGA MKONO RED CARDS YA GIROUD
      • DUNIA YAUMIZA KICHWA UPOTEVU WA NDEGE BILA KUGUNDU...
      • TORRES BADO HAJATULIA
      • FERRY YASHIKA MOTO NA ABIRIA 460 WAHOFIWA KUFA
      • MEHMET ALI AGRA AZURU KABURI LA PAPA JOHN PAUL
      • DUNIA YAUMIZA KICHWA AJALI ZA NDEGE ANGANI
      • MAREKANI YAONGEZA NGUVU KUITAFUTA NDEGE ILIYOPOTEA
      • PILISI TANGA KUENDESHA MSAKO MAJUMBA YA MADANGURO
      • MSIMU WA MAEMBE MOMBASA, WAFANYABIASHARA TANGA WAC...
      • RONALDO, MZUNGU AU MWARABU, CHEKI HAPA PICHA TOFAUTI
      • MAHAKAMA YAMFIKISHA MWANAMKE ALIEGOMA KUMTOA MKE W...
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO NA MAGAZETI YA ...
      • CHEKI PICHAZ TENA ZA HUYO MWANANDINGA, CHRISTIAN R...
      • TAARIFA, HADITHI PUNDE ITAONEKANA
      • SUPA STAA ALICIA KEYS AFURAHIA KUPATA MTOTO CHRISMASS
      • NDEGE ILIYOPOTEA INASADIKIKA KUZAMA BAHARINI
      • DAVIDO AFUNGA MWAKA VIZURI
      • WANIGER WANAKUALIKA HII KATIKA REMIX
      • WATALIKIANA ILA HESHIMA IPO KWA KULINDA WATOTO
      • MKALI HAILEY BALDWIN BADO HAJATULIA
      • MVUA YALETA MAAFA DAR
      • KALA KUACHIA MPYA JANUARY
      • JE, WAIJUA JEZI YENYE KUONGOZA KWA UFUNGAJI?
      • AJIFUNGUA NDANI YA TRENI, ASKARI WA KIUME WASAIDIA...
      • ATHARI YA CHUMVI KATIKA CHAKULA
      • KAKAKUONA AONEKANA TANGA NA DAR
      • VILIO, MAJONZI VYAENDELEA INDONESIA, SALA MAOMBI K...
      • BODABODA AUWAWA KINYAMA KWA KUCHOMEWA NYUMBA AKIW...
      • KISIWA HARISHI
      • SITEGEMEI MUZIKI, NIKO NA BIASHARA BAB KUBWA----,L...
      • ABEBA UJAUZITO WA MWANAE WA KUMZAA MARA MBILI
      • AMUUWA MWANAWE AKIAMINI ATAENDA MBINGUNI
      • JAY Z NA FAMILIA YAKE WANAZUIDI KUINJOY THAILAND
      • NAE YEMI ALADE ASAINI DILI LA MAMILIONI KAMA DAVIDO
      • NICK CANNON ASISISTIZA HATOINGIZA MASHAIRI YA KUMK...
      • SETH ROGEN NA JAMES FRANCO WAVUNJA REKODI YA MAUZO...
      • KANYE WEST AWAFUNIKA MASTAA KIBAO KWA MAVAZI
      • UTAFITI,FURAHA DUNIANI UMEONGEZEKA
      • HIFADHI YA TAIFA YA MKOMAZI YAKABIDHI JENGO LA WOD...
      • HIFADHI YA TAIFA MKOMAZI YAKABIDHI JENGO LA MAMA N...
      • KISIWA HARISHI (22)
      • BABA WA BEYONCE AUZA CD MITAANI
      • SOMA MAKUU YALIYOJIRI MAGAZETINI, TZ
      • colobo zilizofanya vizuri mwa 2014
      • HILARY CLINTON NDIE ANAEPEDWA ZAIDI MAREKANI
      • NICK MINAJ AJUTA KUTOA MIMBA
      • BIBI HARUSI AVURUMISHIWA MAWE AKIWA HOLINI
      • KINARA WA KUINGIZA MADAWA YA KULEVYA ATWANGWA RISA...
      • KANYE WEST ANUNUA JUMBA LA KIFAHARI
      • DULLY SEX ATOA SHUKURANI
      • ACHOMWA KISU KICHWANI NA KUTEMBEA NACHO HADI HOSPITAL
      • RINHANA AMTOA KAKA YAKE KATIKA MAUZO YA CD
      • MOVE ZINAZONGOZA KWA KUIBWA MWAKA 2014
      • OBAMA AWAOMBA RADHWI MAHARUSI HAWA
      • KUFUATIA KUPIGWA RISASI MTUHUMIWA WA MADAWA YA KUL...
      • MIILI YA WAHANGA WA NGEDE ILIYOZAMA BAHARINI YAZID...
      • KISIWA CHA HARISHI (23)
      • KILIO CHA MAJI , WETE PEMBA
      • MAKOBAZI BEI POA
  • ►  2015 (3131)
    • ►  January (417)
    • ►  February (332)
    • ►  March (351)
    • ►  April (308)
    • ►  May (263)
    • ►  June (255)
    • ►  July (260)
    • ►  August (246)
    • ►  September (237)
    • ►  October (210)
    • ►  November (142)
    • ►  December (110)
  • ►  2016 (1913)
    • ►  January (121)
    • ►  February (102)
    • ►  March (131)
    • ►  April (198)
    • ►  May (196)
    • ►  June (197)
    • ►  July (197)
    • ►  August (186)
    • ►  September (159)
    • ►  October (160)
    • ►  November (138)
    • ►  December (128)
  • ►  2017 (562)
    • ►  January (134)
    • ►  February (106)
    • ►  March (113)
    • ►  April (77)
    • ►  May (72)
    • ►  June (11)
    • ►  September (1)
    • ►  October (36)
    • ►  November (10)
    • ►  December (2)
  • ►  2018 (1)
    • ►  February (1)
Picture Window theme. Powered by Blogger.