Wednesday, December 3, 2014

Kweli Kumekucha

Mambo na Vijambo, Sikia hii

Mother carrying her baby on back, Zambia
Hekaheka ya leo imetoka Kunduchi, ambapo mama mmoja amesema alikuwa na mtoto ambaye aliumwa Malaria, baada ya kumuuguza muda mfupi baadaye akafariki ambapo ajabu yake baadaye alikuwa akisikia sauti ya mtoto huyo akilia kwa mbali mara kwa mara wakati wa usiku hali iliyomshangaza na baada ya kuwasimulia marafiki zake wakamwambia kuwa kama anaisikia sauti ya mtoto huyo akilia basi huenda hajafa kweli atakuwa amechukuliwa kwenye mazingira ya ushirikina.
Mama huyo akakutanishwa na mganga ambaye alisema ana uwezo wa kumrudisha mtoto wake na kumtajia gharama ambapo kiasi cha pesa kilichotakiwa kwa kazi hiyo ni shilingi milioni mbili na shilingi mia moja.
Baada ya kukubaliana siku moja alimpigia simu akamwambia aende Mlandizi ambako alimkuta mtoto huyo, ambaye alipomwangalia alithibitisha kuwa ni mtoto wake japo mganga hakumruhusu arudi naye.
Baadaye alipigiwa simu tena na mganga huyo akimwambia aende Kijiji kimoja kilichopo njiani kama unaelekea Dodoma, akapewa mtoto wake lakini ukiangalia picha za mtoto huyo kabla hajafariki na baada ya kurudishwa na mganga huyo inaonekana ni watoto wawili tofauti japo mama wa mtoto anasema huyo ndiye mtoto wake.
Hii ndiyo picha ya watoto hao ambao inasemekana ni tofauti japo mama mzazi anasema ni mtoto mmoja.
Hii ndiyo picha ya watoto hao ambao inasemekana ni tofauti japo mama mzazi anasema ni mtoto mmoja.
Hupitwi na jambo ukifungua Kumekucha blog

No comments:

Post a Comment