Umeisikia hii ya staa anayedaiwa kununua views za video yake kwenye Youtube?
Mwaka
unaisha vizuri kwa baadhi ya wasanii wengine wakitamani hata usiishe
kutokana na mambo kuwanyookea, hii itakuwa kumbukumbu kubwa kwa nyota wa
muziki kutoka Nigeria Yemi Alade, bila shaka ni jina jipya lililowashangaza wengi 2014.
Headline inahusu rekodi ya msanii huyo, unajua kwamba video ya Johnny imetazamwa na watu zaidi ya milioni 10 kupitia mtandao wa Youtube mwaka 2014?
Yemi alishare ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Twitter; “And JOHNNY” hits over 10 million views on VEVO and YouTube in less than a year!!! #KingOfQueens #Johnny’”– @yemialadee
Wapo watu waliotoa comments zao kwenye ujumbe huo kwa kusema kwamba Yemi Alade alinunua views, japo yeye hakujibu chochote kwenye ujumbe huo.
Video hiyo aliiachia miezi tisa
iliyopita, bado haijamaliza mwaka ni miongoni mwa video za nyota wa
muziki kutoka Nigeria zilizotazamwa sana mwaka 2014, ikiwemo Video ya
wimbo wa Davido, ‘Aye’ na video ya wimbo wa kundi la P Square, ‘Personally’ zote kwa pamoja zimetazamwa na watu zaidi ya milioni 10.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment