KUMEKUCHA BLOG
Tanga,CHAMA Cha Wananchi (CUF) Tanga,
kimewataka wananchi waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za
mitaa unaofanyika kesho (leo) kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia
kura.
Akizungumza katika mkutano wa mwisho wa kampeni jana, mgombea
nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Chuda, Suleiman Idd (CUF) aliwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi na kuichagua CUF.
Aliwataka kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kwa amani na
kisha kurejea katika sehemu zao za kujiletea maendeleo na kusubiri matokea na
kuwataka kukipia kura chama hicho kwa wingi ili kuweza kuichukua nafasi hiyo.
“Ndugu zangu wananchi wa Chuda wa CUF na CCM munaonisikiliza
hapa katika mkutano huu wa funga kampeni----nawaomba kwa heshima na taadhima
munipigie kura nyingi ili niwe kiongozi wenu” alisema na kuongeza
“Kwa sera ambazo nimezinadi toka siku ya kwanza ya kampeni
nadhani hakuna chama chengine kilicho na mwelekeo wa kuwaletea maendeleo kama
CUF” alisema Idd
Akiwazungumzia wanawake kujitokeza kwa wingi, mgombea huyo
aliwataka kujitokeza kwa wingi na kuacha shughuli nyengine ili kuweza kumpatia
kura kwa wingi na kuahidi kuwachangia matibabu kwa kila nyumba kaya moja katika
mtaa wake.
Alisema atatoa kipaumbele kwa wanawake wajawazito katika
upatikanaji wa matibu kwa mfumo wa bima ya afya ikiwa na pamoja na wazee
wanaume na wanawake.
“Nikiwa kiongozi wenu wa mtaa jambo la kwanza nitatoa
kipaumbele kwa wanawake wajawazito na wazee katika matibabu kwa nay a biama ya
afya----kila nyumba nitachangia kaya moja” alisema Idd
Alisema katika mtaa wake atahakikisha kila kaya inajiunga na
mfuko wa bima ya afya na kuweza kupata matibabu bure mwaka mzima kwa kuchangia
kiasi kidogo cha fedha.
Alisema pamoja na mambo mengine pia atahakikisha mtaa wake
unakuwa katika mazingira mazuri ya usafi na kuweka sheria ndogo ndogo ili
kuweza kutokomeza magonjwa ya miripuko zikiwemo homa za matumbo na malaria.
Mwisho
No comments:
Post a Comment