Thursday, December 11, 2014

SOMA STORI KUU KATIKA MAGAZETI YA LEO, TZ

Hizi ni Stori kubwa muhimu kwenye Magazeti ya leo Tanzania Desemba 10, 2014


Hizi ni Stori kubwa muhimu kwenye Magazeti ya leo Tanzania Desemba 10, 2014

ln
MWANANCHI
Rais Kikwete jana aliwatunuku nishani Watanzania 28 akiwemo muuza Chips,Kassim Said mwenye miaka28 ambaye alipewa nishani na ushupavu baada ya kupambana na kumdhibiti jambazi mwenye silaha.
Hafla ya utoaji wa nishani hizo ilifanyika jana katika viwanja vya ikulu na kuhudhuriwa na mabalozi na viongozi mbalimbali wa Serikali huku Kassim akiwa kivutio  kutokana na idadi kubwa ya watu kushangazwa na ujasiri wake wa kupambana na jambazi mwenye silaha.
Kijana huyo alikua wa mwisho kutajwa na baada ya mshereheshaji wa hafla hiyo kueleza historia yake kwa ufupi kwamba alizaliwa mwaka 1986,iliibuka minong’ono toka kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo na aliposimulia kisa chenyewe kila mtu aliduwaa.
Akisimulia mkasa huo kijana huyo alisema jambazi huyo alivamia akiwa na bastola huku akiwataka watu wampe fedha  na vitu mbalimbali  na alipoona hakuna aliyemsikiliza alichomoa bastola na kumtishia mmoja wa wateja na hapo ndipo kijana huyo alipoamua kupambana nae na alichukua chepe na kumpiga nalo mara mbili sehemu ya kichwani na kuzirai,na baada alitoa taarifa polisi ambapo walikuja na kumchukua.
MWANANCHI
Siku moja baada ya Ikulu kueleza Rais Kikwete pamoja na kupokea ripoti ya Bunge kuhusu akaunti ya Escrow hawezi kuwachukulia hatua mpaka uchunguzi kuhusu tuhuma hizo utakapokamilika,ofisi ya Rais imesema itafanyia kazi ripoti hiyo ndani ya wiki moja ijayo.
Katibu mkuu kiongozi,Balozi Omben Sefue alisema Rais lazima aagize ripoti maalum kuchunguza na baada ya hapo ndipo atapata mahali pa kuanzia.
“Katika wiki moja ijayo atazitolea uamuzi kwa maana ya kwamba yale mambo yanayomuhusu moja kwa moja atayatolea uamuzi yeye,yake yanayohusu Serikali atayatolea maagizo na maelekezo ya namna ya kuyashughulikia”alisema Semfue.
Rais Kikwete ameelekeza ripoti ya CAG iwekwe hadharani  kwa ajili ya umma kuisoma na kujua ni nini kimesemwa na kupendekezwa na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali.
Rais ameelekeza ripoti hiyo itangazwe kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya kijamii,ili iweze kupatikana kwa Watanzania wengi.
MWANANCHI
Mwanamke mmoja mkazi wa Majengo jijini Mbeya Rose Samuel mwenye miaka 21 juzi alifikishwa mahakamani akidaiwa fidia ya shilingi milioni 1 kwa tuhuma za kufumaniwa na mume wa Mwanahamisi Omari mwenye miaka54.
Katika kesi hiyo Rose anaiomba mahakama ya mwanzo imuamuru mdaiwa huyo kulipa kiwango hicho cha fedha kutokana na kufumaniwa akiwa na mumewe.
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo Onesmo Zunda  atasikiliza kesi hiyo leo baada ya washtakiwa kutoa maelezo ya awali.
Katika maeleo yake ya awali Rose alidai kuwa alimfumania mwanamke huyo usiku wa kuamkia Desemba3 nyumbani kwa mwanaume huyo hata hivyo mshtakiwa alikana  shtaka mahakamani hapo na hakimu kuahirisha kesi akidai hataki kupoteza mda mwingi kufikia maamuzi.
HABARILEO
Siku moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kukaririwa na vyombo vya habari  akisema Katibu mkuu wa Chadema Dk.Slaa anafaa kubeba jahazi la Urais kwa vyama vinavyounda Ukawa,Chama cha Wananchi CUF kimelaani hatua hiyo.
Akizungumza Jijini Dar es salamMkurugenzi wa Habari na uenezi Abdul Kambaya alisema  Kafulila ni mkomavu wa kisiasa hivyo hakupaswa kutoa kauli hiyo.
“Kafulila ni Mkurugenzi wa habari wa NCCR-Mageuzi,ni mtu mwenye ufahamu  wa kutosha na anaweza kupima athari ya jambo analolitolea maoni,kwa hiyo kama kiongozi alipaswa kufahamu athari zitakazojitokeza kutokana na kauli yake”alisema Kambaya.
Alisema umoja huo uliundwa  kupitia wajumbe wa vyama hivyo  kwa lengo la kutetea maoni ya wananchi yaliyowasilishwa katika rasimu ya katiba na tume ya mabadiliko ya katiba iliyokua chini ya Jaji Warioba.
Alimtaka Kafulila na Makamu Mwenyekiti wa Bawacha Hawa Mwaifunga kueleza kikao kilichokaa  na kushiriki katika kutoa mamauzi ya uteuzi huo.
NIPASHE
Kada Maarufu Charles Matawi ya juu aliyekua akitumiwa na CCM katika mikutano yake mbalimbali amekihama chama hicho na kujiunga na Chadema  huku akiteketeza kwa moto sare za chama hicho  katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilayani Tarime.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni  uliohudhuriwa na mjumbe wa Mkutano wa Taifa wa Chadema John Heche,amekua akitumikishwa kama punda na CCM na kugeuzwa daraja la kupandia viongozi wa Chama hicho.
“Nimetumiwa kama punda kubeba mizigo ya viongozi wa CCM,lakini sasa nimegoma kwenda kubeba,hapa nathibitisha kuachana na Chama hicho na nachoma moto sare zao hadharani”alisema kada huyo.
UHURU
Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe ameutaka uongozi wa kampuni ya Reli nchini TRL kuwatumia wafanyakazi wake katika shughuli zake zote badala ya kuweka makandarasi kama ilivyo sasa.
Mwakyembe alitoa mfano wa shughuli za ukarabati ambazo zimekua zikifanywa na kampuni mbalimbali ,ambapo alisema uzabuni wake hauko wazi.
Alisema kuwa ilibainika kuwa wanaoshinda zabuni hizo wengi ni waliokua wafanyakazi wa zamani wa kampuni hiyo,wanaofanyakazi chini ya kiwangona hata mikataba yao haieleweki.
“Mikataba ni ya kiujanjaujanja tu na mingi imekwisha muda wake mingine kiasi cha miaka mitano hadi saba,lakini cha kushangaza bado wanafanya kazi huku wakikodi vifaa vya TRL kwa gharama ndogo isiyo na faida na zaidi kampuni ikiwawekea mafuta.
MTANZANIA
Mwanaume mmoja Ndomo  Mwandu Mkoani Katavi amemkata mkewe Agnes Sikazwe masikio  kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea Novemba 8 mwaka huu majira ya saa sita usiku nyumbani kwa wanandoa hao.
“Kabla ya ugomvi wanandoa hao walikua na ugomvi w amara kwa mara uliokua umedumu kwa muda mrefu na chanzo cha ugomvi huo ni kwamba mwanaume alikua kimtuhumu mkewe kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine kijijini hapo.
Siku ya tukio wanandoa hao walikua wamelala lakini baadaye mwanaume alimvizia mkewe akiwa usingizini na kumkatamasikio huku akilalamika bado anaendelea na mahusiano na mwanaume mwingine.
Baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele kuomba msaada kwa majirani na walipofika eneo la tukio walimkuta akiwa ametapaa damu kila mahali.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, KUMEKUCHA BLOG


No comments:

Post a Comment