Wednesday, December 10, 2014

TUHUMA MAHAKAMANI,

Ni rufaa ya hukumu ya Pistorius na alichokisema baba yake leo Desemba 10

The Judge Reaches Her Verdict In The Trial Of Oscar Pistorius
Mahakama nchini Afrika Kusini imemruhusu kiongozi wa mashitaka kukata rufaa dhidi ya kosa alilopatikana nalo mwanariadha Oscar Pistorius la tuhuma za kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Kesi hiyo, sasa itaanza kusikilizwa katika mahakama ya juu zaidi wakati upande wa mashitaka ukitaka Pistorius ahukumiwe kwa kumuua mpenzi wake kwa kukusudia.
Jaji Thokozile Masipa, alisema hataruhusu rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa ya miaka mitano dhidi ya Oscar mwezi Oktoba.
jaji
Kiongozi wa mashtaka aliyewasilisha kesi ya rufaa dhidi ya Pistorius.
Kiongozi wa mashitaka Gerrie Nel aliiambia mahakama kuwa hukumu hiyo ni ndogo sana ikilinganishwa na kosa la Oscar.
Kwa upande wa baba wa mwanariadha huyo Henke Pistorius alinukuliwa akisema “Mwanangu yupo imara na amekua..kuna vitu vingi katika maisha hivyo anapaswa kujifunza..ingawa hakufanyiwa haki”..
Rufaa hiyo inatarajiwa kusikizwa mwakani
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, KUMEKUCHA BLOG

No comments:

Post a Comment