Sunday, December 14, 2014

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KIZAAZAA

Kumekucha blog
WAKATI wananchi wakisubiria kwa hamu matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliomalizika jioni hii, baadhi ya maeneo yameshuhudiwa kujitokeza vitendo vya uvunjifu wa amani na baadhi ya watu kudiriki kuwaadhibu wanachama pinzani.
Katika mtaa unaojulikana kama msikiti kada mmoja maarufu anadaiwa kumfungia ndani kijana wa chama ambacho kinadaiwa kushinda na hivyo kushangilia kwa kebehi na hivyo kada huyo kushikwa na ghazabu na kumkwida kisha kumsweka ndani.
Hali hiyo ilizusha tafrani na wafuasi wa chama hicho ambacho kinadaiwa kuelekea kushinda ama kilishinda ambapo matokeo rasmi hayajatangazwa hadi muda huu tukiwa mitamboni walikuwa wakishangilia kwa nguvu na kupita mtaa huo zaidi ya mara tano na hivyo kuzusha tafran.
Kule Wilayani Muheza mwandishi wa Kumekucha blog anatuarifu kuwa vituo zaidi ya 21 havikuweza kupiga kura baada ya kutokea malumbano na mabishano ya kivyama na hivyo uchaguzi huo kutofanyika.
Awali kulikuwa na hali tete na kulazimika baadhi ya maofisa usalama kuweka mambo sawa jambo ambalo lilisaidia.
Hakuna taarifa yoyote ya uchaguzi huo.
Fuatilia uchaguzi kupitia kumekucha blog kila wakati

No comments:

Post a Comment