Utaishangaa hii ya kijana aliyefanya upasuaji ili afanane na Kim Kadarshian…
Kijana mmoja mwenye miaka 23 Jordan James Uingereza ameripotiwa kutumia paundi 100,000 za kimarekani sawa na zaidi ya milioni 160 za kitanzania ili afanyiwe upasuaji na kufanana kama mwanamitindo Kim Kadarshian.
Safari yake ya kutaka kujibadilisha ilianza baada ya kumuona Kim Kadarshian katika Tv shoo inayorushwa na kituo cha E news inayojulikana kama Keep Up with Kardashians miaka michache iliyopita na kuvutiwa na mwanamitindo hiyo maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo macho,mdomo pamoja na sura yake na kutamani kuwa kama yeye.
Akizungumzia sababu za kutaka afanane na staa huyo ambaye ni mke wa rapa Kanye West alifafanua kuwa “huwa navutiwa na midomo ya dada huyu na sehemu mbalimbali za mwili wake,nilicheka sana siku niliposikia watu wananitukanakwa nini nimeamua kufanya upasuaji nakuonekana feki,wanadhani mimi nafanya ili nionekana wa kawaida? kama ingekua hivyo ningewaambia madaktari warudishe pesa zangu,”alisema.
Alisema bado hajamaliza matakwa yake na sasa anafikiria kubadilisha pua yake ifanane na mwanamitindo huyo na endapo ataishiwa fedha za kufanya mabadilio hayo yupo tayari kuazima hata kwa familia yake.
“Muonekano wangu mpya kwa watu unanifanya nijisikie fahari kubwa..napenda watu wanavyotumia muda wao kunitazama,kwa wale wote ambao hawapendi muonekano wangu wajue kuna wengine wanapenda.wajue ndio watu pekee ninaowajali pia”alisema.
Ameongeza kuwa Kim Kardashian amekua mtu pekee anayevutiwa nae duniani kote na huwa anaheshimu na kuthamini kazi zake na ndio maana ameweza kutumia muda na fedha zake kutaka kuudhihirishia Ulimwenguni jinsi gani anamkubali.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekuchablog
No comments:
Post a Comment