Thursday, December 18, 2014

AJIFUNGUA PACKING YA TAXI

Pale ambapo mwanamke analazimika kujifungua kwenye parking ya magari eneo la Club…


Pale ambapo mwanamke analazimika kujifungua kwenye parking ya magari eneo la Club…

Parking Lot Sign-313x235
Mwanamke anapokuwa mjamzito hasa unapofika wakati wa kukaribia kujifungua huwa makini sana ili aweze kujifungua salama, lakini kuna wakati ambao hujikuta ana changamoto kutokana na mazingira ambayo uchungu wa kujifungua unampata.
Hii inasikitisha kutokana na kitendo cha mama mmoja kujikuta akilazimika kujifungua katika eneo la parking ya magari nje ya Club kutokana na kupata uchungu akiwa kwenye taxi iliyokuwa ikimpeleka hospitali Tennessee, Marekani.
Maafisa wa zimamoto walipofika eneo la tukio walimkuta mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 akiwa tayari amejifungua na amempakata mtoto wake ndani ya taxi hiyo.
Baadaye mama na mtoto wake walipelekwa Hospitali ya St. Thomas Midtown.
Meneja wa Club ambayo mtoto huyo alizaliwa kwenye eneo la parking amesema wana mpango wa kumpa zawadi mwanamke huyo pamoja na mtoto wake kiasi cha dola 500 pamoja na zawadi nyingine mbalimbali pamoja na toy za kuchezea.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog

No comments:

Post a Comment