Thursday, December 18, 2014

AZIKWA BAADA YA MIAKA KUMI , KENYA



Kutoka Kenya, maiti iliyozikwa baada ya mgogoro wa miaka mitano

Mazishi KnyKatika hali ya kushangaza familia moja ilijikuta katika hali ya furaha kwenye msiba, wakaimba na kucheza ngoma tofauti na ambavyo tumezoea kwamba msibani ni sehemu ambayo watu huwa na majonzi na huzuni.
Furaha hiyo ilitokana na kitendo cha Mahakama kuruhusu mazishi ya ndugu wa familia hiyo huko Kenya baada ya mwili wa marehemu huyo kukaa zaidi ya miaka mitano ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti kutokana na kesi ya mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya marehemu na ndugu yake.
Ardhi ambayo ilikuwa ikigombaniwa ni sehemu ambapo alipaswa kuzikwa marehyemu huyo, hivyo0 kutokana na kesi hiyo wakshindwa kuzika, wiki hii Mahakama kuu ya Nyeri iliruhusu mwili huo kuzikwa eneo hilo ambalo lilikuwa na mgogoro wa muda mrefu.
Kutoka kwenye taarifa iliyoripotiwa na Kituo cha K24, mwanakijiji mmoja alisema; “… sisi tulipanga mazishi huyu kijana hakuweza kuzikwa kwa sababu huyu Mzee alienda kotini na kuweka ile munaita Court Injunction kwamba hawezi kuzikwa katika hili shamba, kwasababu iko na kesi na shamba ni yake kwa hiyo mutu hawezi kuzikwa katika hiyo shamba yake, hiyo ndiyo kesi imekuwa ikiendelea

No comments:

Post a Comment