SIMULIZI
KISIWA CHA HARISHI (12)
ILIPOISHIA TOLEO LLILOPITA
Hakukuwa na aliyemjibu. Sote
tulikuwa tumeshikwa na fadhaa.
“Si niliwambia mtoke
alfajiri, mmelala hadi saa hizi wakati niliwambia kuwa Harishi atakuja leo”
“Ni kweli ulituambia”
nikamkubalia.
“Sasa mbona hamkutoka
alfajiri?’
“Tumepitiwa”
“Mtanilaumu mimi bure
jamani!”
Hatutakulaumu hata kidogo.
Umetufanyia wema sana”
“Harishi alikuja mapema sana akaniambia anasikia
harufu ya kimtumtu. Nikamwambia mtu ni mimi. Akaniambia hebu ngoja. Akatoka kuja
kuwatafuta”
“Siku hizi atakuwa anakuja
kila siku kwa sababu ameona anapata mlo anaoutaka. Ni lazima mjihadhari”
“Mimi naona tuondoke tu humu
ndani” Mwenzangu akasema kwa woga.
“Lakini amekwishakwenda zake.
Kwa leo hatarudi tena” Yasmin akatuambia.
“Itabidi tuondoke tu”
Mwenzangu alizidi kusisitiza.
“Kwani wenzenu wengine wako
wapi?”
ITAENDELEA
“Bado wamelala hadi sasa?”
Yasmin akauliza kwa mshangao.
“Naona bado wamelala”
nikamjibu.
“Kumbe nyinyi hamuwezi kuamka
alfajiri?”
“Tatizo ni kuwa usingizi
wenyewe unakuja wakati wa alfajiri” nikamwambia Yasmin.
“Basi ni balaa. Sasa itabidi
usiku mwende mkalale sehemu nyingine, mjaribu bahati yenu”
“Tutafanya hivyo”
“Kuna nyumba nyingi hazina
watu. Mnaweza kutafuta nyumba nzuri yenye vitanda mfanye makazi yenu.
Hapamtakuwa mnakuja mchana tu, muda ambao nitawambia mimi”
“Tumekue;lewa, ngoja
niwaamshe hawa mabwana”
Tukatoka pamoja mle chumbani.
Tulipotoka tukawaona wenzetu nao wametoka.
“Hivi ndio mnaamka jamani?”
Yasmin akawauliza.
“Dadayetu si unajua usingizi
hautabiriki?” Mtu mmoja akamjibu.
“Hamkumbuki jana
niliwambiaje? Si niliwambia muamke alfajiri muondoke?” Yasmin akawauliza.
“Ni kweli ulituambia lakini
ndio tumepitiwa”
“Shakiri ameuliwa leo na
Harishi!” nikawambia.
“Unasema kweli?” wakaniuliza
kwa pamoja kwa mshituko.
“Ni kwa sababu ya kuchelewa
kuamka. Sisis tumeponea chupuchupu baada ya kuingia mvunguni mwa kitanda”
“Basi utakwisha!”
“Yasmin ametupa wazo. Badala
ya kulala hapa tutafute nyumba nyingine tuweke makazi yetu. Hapa tutakuwa tunakuja
kula chakula mchana katika muda atakaotuambia Yasmin”
“Hivyo itakuwa vizuri” Mmoja
wa wenzetu hao akasema.
“Sasa mjitayarishe, ninaenda
kuwaandalia chai” Yasmin akatuambia.
Wakati Yasmin anakwenda
jikoni, wenzetu wawili waliokuwa wamelala chumba cha pili ilivyokuwa hadi
mwenzetu akauliwa.Tukawaeleza.
Kwa kweli walipata hofu.
“Sasa tukishakunywa chai
tutoke tukatafute hiyo nyumba” nikawambia wenzangu.
Ilipofika saa nne tayari
tulikuwa tumeoga na kunywa chai. Tukamwambia Yasmin tunataka kwenda kutafuta
nyumba ya kukaa kwa maana tayari tulishakuwa wakazi wa kisiwa kile na hatukuwa
na mategemeo ya kuondoka.
“Kwani mpaka mwende
nyote”Yasmin akaniuliza.
“Unataka twende wangapi?”
nikamuuliza.
“Mnaweza kwenda wawili,
wawili mkabaki”
Mimi na wenzangu tukatazamana
lakini sote tulionekana kutoliafikiwazo la Yasmin.
“Acha tu twende sote”
nikamwambia Yasmin.
“Basi ngoja niwasindikize,
msiniache peke yangu”
“Tukizunguka na wewe itakuwa
vizuri” nikamwambia.
“Kwanini?’
“Kwa sababu wewe ndiye
mwenyeji wetu, utaweza kutuongoza vizuri”
“Haya basi twendeni”
Tukatoka na Yasmin. Yasmin
alikuwa akikijua vyema kisiwa hicho. Alituzungusha mitaa mbalimbali tukiangalia
nyumba. Mwisho alitupeleka katiaka nyumba moja ambayo alituambia ilikuwa ya mtu
mmoja tajiri wa kisiwa kile.ambaye naye naye aliuawa na Harishi.
Ilikuwa nyumba nzuri lakini
ilikuwa imechakaa kwa vile ilikuwa haiishi watu. Tulipoingia ndani tulikuta
mavumbi yalikuwa yameenea nyumba nzima.
Tukaanza kazi ya kuisafisha
nyumba. Yasmin alitusaidia kufanya usafi. Ilikuwa kazi iliyotuchukua saa
kadhaa.
Tulipomaliza tulichota maji
kwenye kisima tukaoga kisha tukapumzika. Hapo ndipo tulipoanza kugawana vymba
Nyumba yenyewe ilikuwa ya
vyumba vine na sisi wenyewe tulikuwa wanne. Kila mmoja alijichagulia chumba
chake alichokipenda. Tulifungua makabati tukatoa mashuka na kutandika vitanda
tulivyovikuta humo ndani.
Wakati ninatandika kitanda
Yasmin aliniambia nimpe shuka atandike yeye. Nikampa.
“Natamani sana ningekuwa hapa pamoja na nyinyi” Yasmin
akaniambia wakati anatandika.
“Ukiwa hapa utatuponzea sote”
“Ninasema tu lakini najua
haitawezekana. Unajua katika nyinyi nyote nimekupenda wewe zaidi. Ninatamani
ungekuwa mume wangu”
“Hata mimi natamani ungekuwa
mke wangu lakini ndio tupo jela. Uhai wetu unahisabika”
“Ni kweli. Usikumbushiie
hayo. Tuswali tuombe nusura itufikie”
“Wewe unaswali?” nikamuuliza
Yasmin.
“Ninaswali lakini kwa siri sana. Harishi hataki
niswali. Swala ndiyo inayonipa matumaini ya kuishi”
“Umenikumbusha jambo zuri sana na sisi tutaanza
kuswali”
“Kila mara ninaota kunamtu
atakuja kumuangamiza Harish na mtu huyo atakuwa mume wangu”
ITAENDELEA KESHO, USIKOSE MTU WANGU
No comments:
Post a Comment