Hukumu ya binti aliyemtesa mtoto Uganda imetoka! unajua mahakama imeamua nini? Stori iko hapa
Hukumu imetolewa!Je unamkumbuka yule mfanyakazi
wa ndani nchini Uganda aliyemtesa mtoto? sasa atahukumiwa kifungo cha
miaka minne.
Jolly Tumuhirwe mwenye miaka 22 amehukumiwa
adhabu hiyo baada ya kuthibitika kumtesa mtoto wa miezi minne
aliyejulikana kwa jina la Arnella.
Awali msichana huyo alisema alifanya hivyo ili
kulipiza kisasi baada ya mama wa mtoto huyo kumpiga,hata hivyo mama huyo
alikana kumpiga.
Mwendesha mashtaka Lilian Buchan alimwambia dada
huyo anastahili adhabu hiyo kutokana na kosa hilo la kumtesa kikatili
mtoto asiye na hatia.
Katika video hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya
kijamii na kuthibitika kuwafikia watu zaidi ya milioni 40 iliweza
kumwonyesha binti huyo akimwadhibu mtoto huyo bila huruma huku akitumia
tochi kumpiga sehemu za makalio akiwa hana nguo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment