Tukio la uvamizi Mgahawa uliopo katikati ya Jiji, hali bado tete…
Hali ni tete katika mgahawa wa Lindt
uliopo katikati ya Jiji la Sydney, Australia baada ya kundi la watu
ambao hawajatambulika kuvamia mgahawa huo na kuwashikilia mateka ambao
idadi yao haijafahamika.
Watu watano walifanikiwa kutoka ndani ya
mgahawa huo salama huku kukionekana kupepea bendera nyeusi katika moja
ya madirisha la mgahawa huo ambapo Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott amesema kuna dalili za utekaji huo kuhusishwa masuala ya siasa.
Polisi wameuzunguka mgahawa huo ili kufanya jitihada za kuwaokoa mateka waliokamatwa ndani pamoja na kuwakamata watekaji.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment