Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda, hivi karibuni
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za
Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa
shughuli maalumu.
Waziri
Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu,
ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji,
amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Werema
alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku umma
ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali
waliotajwa katika sakata hilo.
Katika
barua yake ya kujiuzulu, Jaji Werema alisema ushauri wake wa kisheria
kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya
hewa.
Kwa
mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya
mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo
mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi
kurudi nyumbani.
Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.(P.T)
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.
Chadema yakerwa JK kumsifia Werema
Jana,
Chadema kilielezea kusikitishwa kwake na sifa alizotoa Rais Kikwete kwa
Jaji Werema kuwa ni mwaminifu na mwadilifu wakati amejiuzulu kutokana na
kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema kitendo cha Rais kumsifu Jaji Werema kinawakatisha tamaa Watanzania.
"Hakupaswa
kupongezwa badala yake Rais angemwambia kwamba alikuwa kwenye taratibu
za kumfukuza kazi," alisema Mnyika na kuongeza kuwa hata watuhumiwa
wengine katika kashfa hiyo wanaposikia Rais akimpongeza mwenzao wanaona
makosa yao ni jambo la kawaida linaloweza kupongezwa.
"Hata
vyombo vya dola vitaogopa kumshtaki Werema kwa sababu amepongezwa na
Rais kwamba ni mtumishi ambaye alikuwa mwaminifu na mwadilifu," alisema
Mnyika.
Alisema
Watanzania wanasubiri Rais kuwafukuza kazi Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo, katibu mkuu wake, Eliakimu Maswi, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na bodi
nzima ya Tanesco.
"Baada ya kufukuzwa wanatakiwa kushtakiwa," alisema Mnyika.
Taarifa ya nyongeza na Raymond Kaminyoge
niko tayari kukupatia yote yanayojiri kila pembe na tembelea kumekucha blog kila wakati
No comments:
Post a Comment