HADITHI
KISIWA CHA HARISHI (7)
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
“Mimi nasikia harufu ya
binaadamu humu ndani. Kumbe ni wewe!” akamwambia yule mwenzetu aliyemshika
shati. Suati yake ilikuwa ya kuunguruma kama
gari bovu.
Wakati anasema meno yake
yalitoka nje. Yalikuwa meno marefu kama ya
nyani!
Alipomshika mwenzetu shati
alimvuta karibu yake.
“Umeingiaje humu ndani na
umefuata nini….kwanza umetoka wapi?” akamuuliza kwa hasira.
Ghafla Yasmin akatoka.
“Ni nani?” akauliza huku
akimtazama yule mtu ambaye alikuwa akitetemeka.
Yasmin alipomuona alimgundua.
“Itakuwa ni wavuvi
walioharibikiwa na chombo chao, wameona nyumba wameingia wakidhani watapata
msaada” Yasmin akaliambia lile jitu.
“Anaingia humu anamfuata
nani. Huyu simuachi ng’o!” jitu hilo
lilisema na kumshika yule mwenzetu kwenye kiuno kisha likamuinua juu kwa mkono
mmoja na kumgeuza kichwa chini. KIchwa cha mwenzetu kikawa chini ya kichwa cha
jitu lile jitu.
Ndipo jitu hilo lilipokita utosi wa yule mtu kwa ncha ya
upanga wake. Mwenzetu huyo alipiga ukulele mmoja tu “Nakufaaa!” kisha akawa
kimya. Damu ikaanza kuchuruzika kutoka kwenye utosi wakei jitu hilo likakinga mdomo wake
na kuanza kuifyonza!.
SASA ENDELEA
Aliendelea kuinywa ile damu
iliyokuwa ikitoka kama maji ya bomba. Mwisho
alibandika mdomo wake pale kwenye utosi na kuanza kufyonza.
Nilikuwa nikitetemeka kwa
hofu kama niliyepatwa na homa ya baridi ya
ghafla. Nilijua akimalizwa yule mwenzetu itaanza zamu yetu sisi kwani sote
tulikuwa ndani ya lile jumba.
Midomo ya Harishi ilitapakaa
damu. Damu nyingine ilikuwa inavuja midomoni mwake na kuingia kwenye ndevu zake
na kisha kutiririka hadi kwenye kanzu yake.
Yasmin alikuwa ameshika
kichwa chake kwa huzuni na alikuwa amekiinamisha kichwa chake chini ili
asiangalie lile tukio.
Pamoja na huzuni na uchungu
vilivyompata Yasmin bila shaka alikuwa akijiambia “Wameyataka wenyewe.
Nilishawambia waondoke, kumbe wamerudi tena”
Nikaona mafunda ya Harish
yanafutuka huku akitafuna kwa haraka haraka na kumeza. Kumbe alikuwa alikuwa
anafyonza ubongo wa mwenzetu na kuula. Aliula kwa ulafi. Mwingine ulimvuja
midomoni na kuingia kwenye ndevu zake.
Alipotosheka alitupa chini
ile maiti akaanza kujirambaramba midomo na kujifuta kwa mkono. Alipomaliza
aliinama akaushika mguu wa yule mtu aliyemuua.
“Sasa nimeshiba vizuri, ngoja
niondoke” alijisemea peke yake akiuinua ule mguun na kuuburuza kuutoa ule mwili
nje. Aliuburuza huku akiendelea kujirambaramba. Alipofika kwenye mlango aliufungua
na kutoka na ile maiti nje.
Yasmin alikuwa bado amesimama
akimtazama.
“Lakini mimi niliwambia ila
hawakunisikia” akajisemea peke yake huku akitikisa kichwa.
Kwa sababu ya kuzidiwa na
hofu na kujua kuwa sote tutakufa nilijitokeza pale nilipokuwa nimejificha.
Nikamfuata Yasmin.
Yasmin alishituka aliponiona.
“Na wewe umetokea wapi?”
akaniuliza kwa kutaharuki.
“Nilikuwa nimejificha chooni”
nikamjibu kwa sauti ya kutetemeka.
“Unaiona damu hii ya
mwenzenu?”
Yasmin akanionesha damu
iliyokuwa imedondoka chini.
“Nimeiona na nimeona pia
alivyouawa”
“Si niliwambia mwendezenu?”
“Tulirudi
huu usiku tulipoona kuna mvua na hatukuwa na mahali pa kujisitiri”
“Sasa
mmerudi na Harishi ametokea. Mwenzenu ameonekana”
“Kwani
atarudi tena usiku huu?”
“Usiku
huu hatarudi tena lakini kama ameshasikia
harufu zenu anaweza kurudi hata kesho akijua atapata mlo mwingine. Yule hali
kitu isipokuwa damu na ubongo. Watu wa kisiwa chote hiki amewamaliza yeye na
ana nguvu zisizo za kawaida. Yule mtu amemuinua juu kwa mkono mmoja tu”
“Na
amempeleka wapi?”
“Amekwenda
kumtupa nje ili asubuhi aliwe na kunguru”
“Sasa
sijui sisi tutakimbilia wapi kwani chombo chetu kimekataa kabisa kuwaka”
“Mimi
sina la kuwambia kwani popote mtakapokwenda ndani ya kisiwa hiki atawagundua na
atawamaliza mmoja mmoja”
Nilibaki
kuduwaa na kutikisa kchwa. Kwa mara ya kwanza niliona kazi ya uvuvi ilikuwa
mbaya. Laiti kama ningejua kuwa chombo chetu kingeharibika baharini
nisingeshiriki katika safari ile.
“Wenzako
wengine wako wapi?” Yasmin akaniuliza.
“Nikwambie
ukweli Yasmin, sisi tulirudi mapema huu usiku tukaigia jikoni na kula chakula
chako kwa sababu tulikuwa na njaa. Tukaingia vyumbani kulala. Sasa tulitoka
watu wawili kuja kujisaidia. Huku nyuma mwenzetu mmoja naye alitoka peke yake,
Ndiye yule aliyekamatwa na kuuawa”
“Wenzako
wengine wako wapi?”
“Mmoja
amejificha chooni na wenzetu wengine wako vyumbani”
“Sasa
na nyinyi nendeni mkalale, asubuhi mtafanya maarifa. Yule jini hatarudi kwa
leo, ameshashiba”
Yule
mwenzangu aliyekuwa chooni aliposikia maneno yale alitoka haraka. Yasmin
akamtazama.
“Nyinyi
mna bahati sana.
Angeweza kushikwa mmojawenu”
“Ni
kweli kwa sababu sisi ndio tuliotoka kwanza” nikamwambia Yasmin.
“Basi
nendeni mkalale”
Tukarudi
kwenye vile vyumba. Yasmin alikuwa bado amesimama akituangalia hadi
tulipofungua mlango na kuingia chumbani’
Wala
hatukulala kamwe. Mimi nilikaa macho usiku kucha nikimuwaza yule mwenzetu
aliyeuawa kikatili.
“Nyinyi
mna bahati sana.
Angeweza kushikwa mmojawenu…” nikawa nayakumbuka maneno ya Yasmin huku mwili
ukinisisimka kwa hofu.
No comments:
Post a Comment