Wednesday, December 10, 2014

NANI MKALI LEOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Nani Mkali kati ya Ronaldo na Messi?

1137334-18372662-1600-900
Upinzani kati ya wachezaji wawili nyota duniani Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni kitu kinachozungumzwa sana kwenye vyombo vya habari .
Wachezaji hawa wamekuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora wao hali inayosababisha ubishi wa nani mkali kati yao kuwa mkubwa sana kila mara unapotokea .
Kila mmoja kati ya wachezaji hawa ana rekodi ya kipekee linapokuja suala la ufungaji wa mabao kwa timu zao na zaidi katika miaka mitano iliyopita wachezaji hawa wamekuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia wakiwa wanapewa nafasi sawa ya kutwaa tuzo hiyo .
Ronaldo na Messi wamekuwa wakipambana kila mmoja akionekana kuwa bora kuliko mwenzie .
Ronaldo na Messi wamekuwa wakipambana kila mmoja akionekana kuwa bora kuliko mwenzie .
Msimu huu Ronaldo anaonekana kama anamzidi Messi hasa kwenye ufungaji wa mabao ambapo hadi sasa Mreno huyo amefunga mabao 30 huku Messi akiwa na mabao 20 kwneye mashindano yote .
Pamoja na kuzidiwa kwa mabao 10 Ronaldo anaonekana kuwa na wakati mwepesi zaidi kufunga mabao yake ambapo mabao tisa kati ya kumi ambayo anamzidi nayo Messi amefunga kwa mikwaju ya penati huku Messi akiwa hajafunga idadi kubwa ya mabao ya penati .
Ronaldo amefunga mabao 30 kwenye mechi 22 ambapo amefunga mabao tisa kwa njia ya penati na katika mabao hayo amefunga Hat-Trick 4 yaani mara ambazo amefunga mabao matatu amefanya hivyo mara nne .
cristiano-ronaldo-vs-lionel-messi_136wouu8j1ryt18g00d3vykhr7
Kwa upande wa Messi amefunga mabao 20 kwenye mechi 19 ambapo amefunga hat-trick mara tatu na kati ya hayo hajafunga penati hata moja .
Katika mbio za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka huu Ronaldo anaelekea kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo baada ya kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka huu .

No comments:

Post a Comment