Mashirikayasiyo ya Kiserikali yafungiwa, yahusishwa kushirikiana na magaidi
Mashirikayasiyo ya Kiserikali yafungiwa, yahusishwa kushirikiana na magaidi
Serikali ya Kenya jana December 16
ilitangaza kyafutia leseni mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 510,
kutokana na kutofuata kanuni za Mashirika hayo huku mengine 15 yakifutwa
kutokana na kusemekana kuwa yanahusika kufadhili shughuli za kigaidi
nchini humo ambapo maelfu ya wafanyakazi wakiwa na wasiwasi wa kukosa
ajira.
Taarifa kutoka Kenya zinasema kuwa
mashirika mengi yamekuwa yakikiuka kanuni zilizowekwa ikiwa ni pamoja na
kutumia njia inayofaa kupata vibali vya wafanyakazi wanaotoka nchi za
nje na pamoja na kuipa Serikali nakala ya matumizi ya fedha wanazopata
kutoka kwa wafadhili.
Hatua hiyo inaonekana kama juhudi za Serikali kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini humo huku uchunguzi ukiwa unaendelea.
No comments:
Post a Comment