Mbali na vioja vya Solange, Beyonce kathibitisha kuwa yeye nini dada bora
Alichokifanaya mwimbaji nyota Beyoncé
Knowles-Carter, kwa mdogo wake Solange Knowles, kimeudhihirishia
ulimwengu ni kwa kiasi gani yeye ni moja ya ndugu na dada bora.
Kwa mfano ingekuwa Bongo lile noma
ambalo alilifanya Solange kwa shemeji yake, Jay Z huenda undugu
ungeishia pale kati ya dada mtu na mdogo wake, haijawa hivyo kwa Queen
Bey, ameendelea kushow love kubwa kubwa kila kunapokucha.
Maisha yanaendelea poa kwenye familia hiyo, Beyonce ameshaweka dola nyingi sana kuanzia kwenye honeymoon ya mdogo wake ambayo wazee wa udaku wanasema eti vacation ya Solange na Ferguson kule Brazil ni dada Bey ndiye aliyefadhili kila kitu!
Hakuishia hapo, mpya ikufikie kwamba
Beyonce amempa Solange zawadi ya safari ndani ya Boti ya kifahari, first
class ambayo ina huduma zote muhimu, dada huyo wa nguvu anaamini mdogo
wake anastahili kila aina ya zawadi kwa kuwa kampata mume ambaye alikuwa
akimhitaji kwa maisha yake yote.
Kweli mwenye mkono wa kutoa hupokea pia,
Beyonce hana hasara yoyote kwa zawadi hizo kwa Solange, unakumbuka ile
shopping iliyomwendea mtoto wa Kelly Rowland? Titan ambaye
ni mtoto wa kwanza wa Kelly Rowland, alienjoy zawadi toka kwa shangazi
Bey, kitanda very special kilichochorwa jina la mtoto huyo kwa madini ya
dhahabu, suti na jacket la leather na pampers za Luis Vuitton, thamani
ya vyote sio chini ya dola laki tatu.
Akikusanya kile alichokivuna mwaka huu
2014, ambacho ni kama dola milioni 115 kwa mujibu wa Forbes kiukweli ni
kama hana alichokipoteza hata kidogo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,kumekucha blog
No comments:
Post a Comment