Zimeanza tetesi na swali likafuatia, Marcio Maximo anaondoka Yanga ?
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo huenda akaondoka ndani ya klabu ya Yanga kufuatia kushindwa kuelewana na uongozi wa klabu hiyo .
Habari zaidi zinasema kuwa kocha huyo
amefikia hatua ya kuanza kuwaaga baadhi ya wachezaji alio nao karibu
akisema kuwa anaondoka kwani amekiri kuwa ni vigumu kuiongoza klabu ya
Yanga.
Hali ilianza kuwa ngumu kwa Maximo baada
ya kocha huyo kuishuhudia timu yake ikifungwa kwenye mchezo wa Mtani
Jembe dhidi ya mtani wake wa jadi Simba .
Inasemekana kuwa kikosi alichokipanga
Maximo kwenye mchezo huo ambacho kilionekana kuwa cha kujihami sana kama
ambavyo imetokea kuwa kawaida ya Mbrazil huyo kwenye mechi kubwa
kilizua minong’ono miongoni mwa wachezaji wake hali ambayo ilifanya
viongozi wa timu hiyo kutopendezwa na timu hiyo kufungwa 2-0.
Maximo inadaiwa amepinga kitendo cha
uongozi wa Yanga kuwa na mpango wa kumuajiri mkurugenzi wa ufundi
akiamini kuwa anapaswa kupewa uhuru wa kufanya kazi yake bila kuingiliwa
na mtu .
Tetesi zaidi zinasema kuwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Mholanzi
Hans Van Der Pluijm tayari yuko nchini Tanzania na ameandaliwa kuchukua
mikoba ya Maximo endapo Mbrazil huyo ataamua kuondoka kama ilivyoanza
kusikika .
No comments:
Post a Comment