Uganda In Burundi Out ndani ya Simba Sc.
Ni kama vile klabu ya Simba ina mapenzi
na taifa la Uganda baada ya klabu hiyo kukamilisha jumla ya wachezaji
watano raia wa kigeni ambao wanatoka kwenye taifa hilo la Afrika
Mashariki .
Simba imetangaza na kuthibitisha kuwa
wachezaji wake watano wa kigeni kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi, Daniel
Serunkumma, Simon Serunkumma, Joseph Owino na Juko Mursheed.
Wachezaji wawili kati ya hao (Okwi na
Owino ) na watatu wengine (Serunkumma Simon, Dany na Juko) wamesajiliwa
katika kipindi hiki ambapo dirisha dogo la usajili liko wazi.
Nafasi za wachezaji watatu hao raia wa
Uganda zimekuja kujaza nafasi za wachezaji wawili toka Burundi ambao ni
Amisi Tambwe na Pierre Kwizera pamoja na Mkenya Paul Mungai Kiongera .
Kiongera bado ataendelea kuwa mchezaji
wa Simba hadi atakapopona jeraha lake la goti ambapo amekwenda kufanyiwa
upasuaji nchini India huku Tambwe na Kwizera wakiwa wameachwa moja kwa
moja .
No comments:
Post a Comment