Usiache kupitia undani wa Stori kubwa muhimu kwenye Magazeti ya Tanzania leo December 4,2014
NIPASHE
Sakata ya wizi wa mabilioni ya fedha za akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo benki kuu ya Tanzania ‘BoT’ limeendelea kushika kasi baada ya Chama cha wananchi CUF kung’ang’ania Waziri mkuu Mizengo Pinda anapaswa kuwajibishwa.
Mwenyekiti wa CUF Taifa Ibrahim Lipumba amesema Rais Jakaya Kikwete anapaswa achukue hatua kali za kumwajibisha Pinda kwa kutengua uteuzi wake kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwakani ili nchi iweze kuwa na uchaguzi wenye amani na haki.
Alisema kama Kikwete hatachukua hatua za kumwajibisha Pinda na viongozi wengine waliohusika na wizi huo,Chama chake kwa kushirikiana na Umoja wa Vyama vya siasa ‘Ukawa’ watafanya maandamano ya nchi nzima kushinikiza waondolewe.
Alisema ni jambo la kushangaza kuona viongozi waliotajwa katika kashfa hiyo wanaendelea kuwepo katika ofisi za umma bila kuwajibika hali inayotia mashaka kuwa wanaweza kufanya njama za kubadilisha nyaraka ili kupoteza ushahidi.
“Rais Kikwete kama anataka uchaguzi uwe huru na waamani achukue maamuzi magumu ya kuwawajibisha wahusika wote waliotajwa katika wizi huo akiwemo Waziri mkuu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Oktoba mwakani,”alisema Lipumba.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa iliyokua tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba juzi alifanya mazungumzo ya saa2 na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali PAC Zitto Kabwe kuhusu mausuala ya uongozi na uwajibikaji baada yaMbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kumtembelea nyumbani kwake Masaki,Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo Zitto pia alimweleza kuhusu uchotwaji wa shilingi bilioni306 katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Kukutana na kingozi huyo kumekuja ikiwa zimepita siku mbili tangu Warioba alipozungumza na Gazeti hili kuhusu sakata la Escrow na maazimio manane ya Bunge.
Zitto alimtembelea jaji Warioba kitendo kilichotafsiriwa kama Mbunge huyo kutolea ufafanuzi maoni ya jaji Warioba katika ripoti hiyo licha ya kuwa yameonekana kuhusika katika kashfa hiyo.
MWANANCHI
Mmiliki wa kampuni ya kufua umeme yaIPTL Habirnder Seth amesema anafikiria mara mbilimbili iwapo ataendelea kuwekeza nchini au la, baada ya kuwapo kwa tuhuma kuwa alihusika na uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
“Nimeongelewa sana kiasi kwamba nimeona hakuna amani ya kuwekeza Tanzania,nitajifikiria marambilimbili,wananchi wanaelewa vingine kabisa kuhusu suala hili kwa sababu ya upotoshwaji,”alisema.
Sett ambaye anatuhumiwa kujipatia asilimia70 ya hisa katika kampuni ya IPTL isivyo halali alisema hafikiri kuwekeza zaidi nchini kwa sababu yakuwapo maneno mengi na shutuma zilizo na ukweli,zilizoelekezwa kwake kuhusu sakata hilo.
Kauli hiyo ya bosi wa IPTL imekuja wakati Taifa likisubiri utekelezaji wa maazimio manane yaliyotolewa na Bunge dhidi ya ufisadi wa sakata la Escrow.
MTANZANIA
Baadhi ya madereva wamebainika kutokua na sifa ya kuendesha magari ya abiria na mizigo kutokana na kuwa na tatizo la kushindwa kuona mbali.
Zoezi hilo lilifannywa likihisishwa na madereva kutoka Mikoa ya Morogoro,Pwani,Arusha kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani hapa nchini.
Kamanda wa Polisi kitengo cha Afya Paul Kabogo alisema madereva hao walipimwa shinikizo la damu,macho,kisukari,malaria,uzito na Ukimwi.
Wengi wa madereva hao walibainika kuwa shinikizo la damu,matatizo ya kutoona mbali pamoja na kisukari na kushauriwa kuwa wanapima mara kwa mara ili kubaini magonjwa mapema kabla na baada ya safari.
MTANZANIA
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kurukekere katika Wilaya ya Bunda wanafanyishwa kazi za vibarua mashambani na walimu ili kupata fedha za kununulia chaki za kufundishia kitendo ambacho kimelalamikiwa vikali na wananchi.
Wakitoa malalamiko yao wananchi hao walisema wanafunzi wamekua wakitumia muda mwingi kufanya kazi za vibarua zikiwemo za kulima mashamba ya watu binafsi wakati wa vipindi vya masomo ikiwa ni pamoja na kutembea umbali mrefu kwenda kwenye mashamba hayo.
Walisema baada ya kuona watoto wakiwa kwenye mashamba hayo walikwenda kuwahoji walimu wao na walijibiwa kwamba wanafanya hivyo ili zipatikane fedha za kununulia chaki na mahitaji mengine ya shule hiyo.
Aidha walisema hali hiyo imewafanya wanafunzi kukosa muda wa kusoma na kuchangia kusuka kwa kiwango cha ufaulu kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka ya nyuma.
MTANZANIA
Tanzania inatajwa kuwa moja ya nchi 40 duniani zilizokithiri kwa tatizo la mimba za utotoni.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Idadi ya watu duniani UNFP.
Akitoa mada katika maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mary Massay alisema sababu zilizotajwa kuchangia mimba za utotoni ni pamoja na kukithiri kwa tatizo la ndoa za utotoni.
“Tanzania ni moja ya nchi zenye viwango vya juu sana vya ndoa za utotoni duniani kwani takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka18 huku asilimia 37 ya wanawake wenye miaka 20 hadi 24 waliolewa au kuwekwa ndani kinyumba kabla ya kufikisha umri wa miaka18,”alisema Massay.
Hata hivyo aliwataka wazazi wasikubali kuwa mawakala wa ndoa za utotoni kwani zinawaathiri wasichana na wanawake kwa kuwanyima haki za msingi kama elimu na kuhatarisha maisha wakati wa kujifungua.
HABARILEO
Vyama vinne vya siasa vilivyoungana na kuunda Umoja wa Ukawa Mkoani Arusha vimeshindwa kuachiana nafasi ya Uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba14.
Vyama vyote vinne vimesimamisha wagombea katika mitaa ndani ya Mkoa wa Arusha kinyume na makubaliano waliyosaini na viongozi wao hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Kitendo hicho kimeifanya CCM kutwaa kiulaini uongozi kwenye vijiji 183 kati ya 406 na kimeweza kushinda kwa rufaa mitaa sita kati ya 155 ambapo Mkoa mzima una vijiji 406 na mitaa 155.
Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Kaskazini Aman Golugwa alisema makubaliano ya viongozi wa Ukawa bado yapo pale pale na alikiri vyama vinavyoundwa na Ukawa Mkoani humo kusimamisha mgombea kila mmoja kivyake lakini akasisitiza kuwa hiyo haina maana makubaliano yao ya kushirikiana yamevunjika.
HABARILEO
Mahakama inaangalia uwezekano wa kuruhusu vyombo vya habari kurekodi picha na sauti kuwezesha vituo vya redio na Televisheni kuripoti habari za mahakama wakati kesi zinaendelea.
Jaji Mkuu Othman Chande alisema mahakama inajifunza kutoka kwa nchi zinazoruhusu vituo vya redio na televisheni kuripoti habari wakati kesi inaendelea.
Alisema utaratibu huo utaanza kwa kuripoti kesi za madai zenye mvuto kwa jamii na kwamba utaratibu mzima unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa baada ya mahakama na vyombo vya habari kukaa pamoja juu ya maadili,uhuru na mipaka ya muhimili ili kuondoa migongano wakati wa kuandika na kuripoti habari za mahakama kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Hivi sasa waandishi wa habari hawaruhusiwi kupiga picha za video wala kurekodi sauti wakati kesi zikiendelea badala yake wanaruhusiwa kuandika habari hizo kisha kuripoti kile walichoandika bila kuonyesha mwenendo mzima wa kesi kwa kutumia sauti na picha za video.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Kumekucha blog
No comments:
Post a Comment