Monday, December 15, 2014

SIMBA YAMSAJILI HASSAN KESSY

Simba yaongeza nguvu kwa kusajili beki, unajua anatoka timu gani?


Simba yaongeza nguvu kwa kusajili beki, unajua anatoka timu gani?

simba_logo_med_hr
Katika usiku wa jana ambao umekuwa na movement nyingi za wachezaji na makocha , klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni toka timu ya Mtibwa Sugar, Hassan Kessy.
Beki huyo ambaye ametokea kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kutumainiwa kwenye klabu hiyo ya wakata miwa wa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro, anaungana na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Simon Sserunkuma, Danny Sserunkuma, na Juko Murshid wote kutoka Uganda.
Kessy ambaye ametajwa kuwa moja kati ya wachezaji wanaokaribia kuwa mmoja ya wachezaji wa Timu ya Taifa Stars alichezea Mtibwa kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki ambao ilifungwa na Azam Fc 3-1.
hassan kessy
Beki huyu anasajiliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa Simba wakiongozwa na Geoffrey Nyange Kaburu na Kiongozi wa Mtibwa, Jamal Bayser.
Tetesi zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni 30.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog

No comments:

Post a Comment