Breaking news ya kocha Marcio Maximo kuondoka Yanga.
Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi
wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba aada ya kushindwa
kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya
ufundi.
Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri
Mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo
ambalo Maximo hakukubaliana nalo.
Tukio hili linaendeleza historia ya
Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani
Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia
kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog
No comments:
Post a Comment