Mkusanyiko wa Stori kubwa muhimu kwenye Magazeti ya leo Tanzania, Desemba 5, 2014
HABARILEO
Mkazi wa kijiji cha Chibwechagula Mkoani Dodoma Ruth Matonya mwenye umri wa miaka 26 amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nusu ya sura yake inafanana na chura na nusu nyingine inafanana na binadamu.
Mtoto huyo alizaliwa katika kituo cha afya cha Mtakatifu Luka kinachomilikiwa na kanisa la Anglikana alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Edwin Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufika katika kituo hicho alikua na uchungu ambao haukua na kikomo lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida licha ya njia ya uzazi kufunguka.
Alisema kutokana na hali hiyo iliwalazimu kumfanyia upasuaji mama huyo kwa lengo la kuokoa maisha yake na mtoto na mara baada ya upasuaji waliweza kutoa mtoto mwenye jinsia ya kike ambaye alikua na sura isiyoeleweka na sura yake nusu ilikua na binadamu na nyingine ya chura.
HABARILEO
Katika kuhakikisha uchochezi unaoharibu amani ya nchi Unathibitiwa wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa,Serikali imeagiza Mamlaka ya sekta ya Mawasialino nchini TCRA kuja na mwongozo wa Mamlaka za simu katika kuthibiti ujumbe mfupi kwa njia ya simu.
Waziri wa Mawasiliano Makame Mbarawa alisema ujumbe mfupi kwenye simu usipothibitiwa unaweza kuleta madhara makubwa wakati wa uchaguzi.
“TRCA mje na mwongozo wa makampuni ya simu hasa kuhusu ujumbe wa simu maana kama itaachwa hivi hivi wakati wa uchaguzi itakua ni hatari,Kenya ilifanya hili na ikafanikiwa,”alisema Mbarawa.
Tayari TCRA imeandaa miongozo ya namna ya kuripoti na kuandaa vipindi wakati wa uchaguzi kwa upande wa sekta ya utangazaji na wamiliki wa mitandao ya kijamii.
MWANANCHI
Harufu ya kuisha kwa mgogoro baina ya Zitto Kabwe na Chama chake cha Chadema inanukia,lakini Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anataka kuwepo na mazungumzo kubaini tatizo ili atakayebainika kuwa alifanya makosa awe tayari kuomba radhi hadharani.
Zitto alikiri Mbungeni kuwa amekua akimis harakati zilizokua zikifanywa na vyama vya upinzani wakati wa Bunge maalum la Katiba,harakati zilizozaa Umoja wa Katiba ya wananchi na kufurahia kuhudhuria mara kwa mara vikao vya umoja huo.
Zitto ambaye Novemba mwaka jana alivuliwa nyadhifa ndani ya Chama hicho kwa madai ya kukihujumu Chama alifanikiwa kulinda uanachama wake baada ya kufungua kesi mahakamani na kufanikiwa kupata amri ya kuzuia asijadiliwe..
“Ukweli wangu ndani ya Chadema ni nini?mimi ninaona sina kosa lolote ndani ya Chadema,ninachotaka mimi nielezwe ukweli bila chembe ya shaka,Nitakua tayari kuomba radhi hadharani kama ikibainika nilifanya makosa na kama ikibainika Chama kilifanya makosa,nacho kiwe tayari kuomba radhi hadharani na ukweli uwe mbele katika maridhiano”alisema Zitto.
MWANANCHI
Shirika la Polisi la kimataifa Interpol imewapigia magoti Watanzania ikitaka msaada wao katika kumsaka mtuhumiwa wa kwanza wa kesi ya utoroshwaji wanyamapori hai 100 kwa ndege ya jeshi ya Pakistan kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA.
Hii ni mara ya kwanza kwa Interpol kuomba msaada huo baada ya mtuhumiwa huyo Ahmed Kamrani kutoweka baada ya kubainika kuwa anasakwa kwa tuhuma za kutorosha wanyama hao kwa msaada wa raia wa Tanzania ambao baadhi yao wamekamatwa na kesi inaendelea mjini Moshi.
Shirika hilo limetoa orodha ya watu tisa ambao limewaelezea kuwa ni waharibifu wa mazingira kwa kuhusika kwenye utoroshaji huo wa wanyama,wakiwemo Twiga wanne na ndege wa aina mbalimbali,uliofanyika Novemba 24,tukio ambalo Interpol wamelifananisha na hadithi ya Nuhu kuingiza viumbe kwenye safina kabla ya gharika.
Interpol imefikia hatua ya kuwatafuta maharamia hao kwa udi na uvumba katika operesheni kubwa iliyoanzishwa Oktoba mwaka huu ikiwalenga watuhumiwa wa uharamia ziadi ya 139 kati ya nchi36 kote duniani ikiwemo Tanzania.
MWANANCHI
Zaidi ya nusu ya Watanzania wamekata tamaa ya maisha badala yake wanafikiria hali zao zitakua bora baada ya miaka10 ijayo,
Kutokana na kukata tamaa wananchi wa maeneo mbalimbali wamepoteza hata hamu ya kutumia haki zao za msingi kama kushiriki katika kuchagua viongozi wao wa ngazi mbalimbali kwa mujibu wa utafiti wa Twaweza.
Utafiti huo ulifanywa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania bara mwezi Agasti kwa kuhoji watu 1,408 ambapo Watanzania wanaamini kuwa maisha yao yatakua bora mpaka kufikia mwaka 2025.
Baadhi ya wananchi bado wana wasiwasi na karibu mwananchi mmoja kati ya watano anahofia maisha yake yatakua mabaya zaidi mwaka 2025 kuliko yalivyo leo na wapo wengine wanaodhani nchi itakua mahali pabaya pa kuishi ifikapo mwaka 2025.
MWANANCHI
Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Utabibu Moshi amejifungua mtoto katika choo cha Hospitali ya rufaa KCMC na kisha kumtupa mtoto wake kwenye kasha la takataka.
Tukio hilo ambalo limezua gumzo kubwa mjini Moshi lilitokea juzi asubuhi katika choo kilichopo mapokezi ya wagonjwa waliozidiwa.
Habari kutoka katika hospitali hiyo zinasema mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa jina lake limehifadhiwa ambaye anasoma mwaka wa kwanza anasomea masomo ya matibabu yamazoezi ya viungo.
Mwanafunzi huyo alifika eneo la mapokezi akiwa na mwanafunzi mwenzake na akaingia chooni kwa lengo la kujisaidia na baada ya muda muhudumu wa usafi aliingia na kukuta choo kimetapakaa damu na baadaye kusikia sauti ya mtoto akilia kutoka kwenye pipa la taka lililopo ndani ya choo hicho.
Alipochungulia alikutana na mtoto mchanga ambaye alikua hata hajakatwa kitovu na inasemekana mwanafunzi huyo alikwenda pale baada ya kusikia ana maumivu ya tumbo na kwa sasa wanamshikilia na uongozi wahospitali kwa uchunguzi zaidi.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, Kumekucha blog
No comments:
Post a Comment