Alichokiandika Bill Cosby kuhusu shutuma za kubaka zinazomkabili
Watu wengi walionekana kumlaani Cosby
kuhusiana na shutuma zinazomkabili lakini wapo wachache ambao walisimama
upande tofauti ambapo ndiyo waliompa nguvu ya kutweet akiwashukuru kwa
kuonyesha kumpa moyo.
Cosby alitweet akiwashukuru Whoopi Goldberg na Jill Scott
ambao walieleza kwa nyakati tofauti namna ambavyo hawakupendezwa na
kitendo cha vyombo vya habari kueneza kashfa za ubakaji juu ya Cosby.
Cosby hakuwahi kuzungumza hadharani
kujibu chochote kuhusiana na shutuma hizo za ubakaji, japo shutuma
zinazozungumziwa sasa zinafanya idadi ya wanawake ambao wamewahi
kuripoti kuhusu kufanyiwa hivyo kufikia 20.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, Kumekucha blog
No comments:
Post a Comment