Sunday, December 14, 2014

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA TANGA WAGUBIKWA NA VURUGU



Kumekucha blog
Tanga, ZOEZI la uhesabuji kura Serikali za mitaa katika vituo mbalimbali halmashauri ya jiji la Tanga limegubikwa na vitimbi vya uvunjifu wa amani na kulazimika vyombo vya usalama kuingilia kati.
Katika kituo cha upigaji kura cha Madina halmashauri ya jiji la Tanga mtu mmoja ambaye hakujulikana jina alichukua sanduku la kupiga kura na kuzimwaga chini hali ambayo ilizusha tafrani na baadhi ya watu kupigana.
Jeshi la polisi lilifika na kurejesha usalama na zoezi kuendelea huku kukiwa na ulinzi wa askari polisi wakiwa na silaha za kuzuia vitendo vyovyote vya uharibifu wa amani.
Tukio hilo limedaiwa kufanyika baada ya mwanachama huyo kuona chama chake kuona mazingira ya kuelemewa na hivyo kukimbilia sanduku la kura na kulitupa chini hali iliyozusha kizaazaa.
Katika kituo cha Mikanjuni mama mmoja alimpiga mtoto wake baada ya kukaidi kupiga kura kwa madai kuwa zoezi hilo lilitawaliwa na vitendo vya vurugu na mamluki na baadhi ya watu kupiga kura zaidi ya mara moja.
Tukio hilo lilitokea wakati mama huyo ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake, alisema aliweza kufika katika kituo chake cha kupigia kura toka alfajiri lakini hadi kufikia saa 9 mchana jina lake halikutajwa na hivyo kuwataka watoto wake nao waondoke katika kituo hicho.
“Jina langu katika ubao lipo na ni la mwanzo mwanzo chakushangaza wenzangu ambao wamekuja muda kuchelewa wanaingia ndani na kupiga kura na kuondoka---mimi napigwa na jua hadi muda huu” alisema
“Kwa ukiritimba huu bora mimi na watoto wangu sote tusipige----uamuzi wa kumpiga ni kukaidi agizo langu na ndio nikachukua uamuzi wa fimbo” alisema
Wakati wa zoezi la kupiga kura wananchi wengi wamelalamikia mfumo wa kuita  majina na kuacha utaratibu uliozoeleka wa foleni na hivyo kuzusha hali ya sitofahamu.
                                             Mwisho    

No comments:

Post a Comment