Sunday, December 14, 2014

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA VURUGU TUPU

Waandishi wetu mjini na Wilayani, Kumekuchablog
Tanga, Uchaguzi Serikali za mitaa unaoendelea nchini kote leo unaendelea licha baadhi ya maeneo kugubikwa na dosari kikiwemo kituo cha kupigia kura cha kijiji cha Ubembe Wilayani Muheza Mkoani Tanga wapiga kura kushindwa kukamilisha adhma yao baada ya vifaa vya kupigia kura kutowasili eneo hilo.
Mbali ya wapiga kura kufikia eneo la kupigia kura mapema ili kuwahi na kurejea katika majukumu mengine ya uzalishaji mali imekuwa tofauti na hivyo kupigwa na jua na baadhi yao kurejea majumbani kwao.
Akizungumza na Kumekucha blog mkazi wa Ubembe, Suleiman Omary, alisema uchaguzi huo ni ishara kuwa mwaka 2015 uchaguzi mkuu unaweza kuwa kama wa Serikali za mitaa na hivyo kuingiwa na hofu ya kutofanyika kwa amani na utulivu.
Katika jiji la Tanga wapiga kura wengi wamekuwa wakilalamika mfumo ambao unatumika wa kuita majina ambao ni utaratibu tofauti na uliozoeleka kwa kupanga foleni.
Mmoja wa wapiga kura kituo cha Chumvini ambaye hakutaka kutaja jina lake ameiambia Kumekucha blog kuwa hakuna maana ya kufika mapema vituoni kwa mfumo huo wa kupiga kura na hivyo ni vyema kurejea majumbani na kujikalia hadi muda wa jioni.
"Mimi nimefika saa 12 na kuwa wa kwanza lakini hadi muda huu wa saa 7 jina langu halijatajwa---kuna maana gani ya kuja mapema ni bora nijirejee nyumbani" alisema
Ameitaka tume ya uchaguzi kubadilisha mfuo huo na isije kufanya katika uchaguzi mkuu mwakani vyenginevyo watu wengi hawatoweza kujitokeza kupiga kura.
Katika kata ya mabawa eneo la Mikanjuni vurugu kubwa imejitokeza baada ya wafuasi wa CUF na CCM kutishiana misuli kwa kile kilichodaiwa kuwa kila chama kinakituhumu mwenzake kupandikiza mamluki na hivyo kulazimika jeshi la polisi kutumia nguvu ya ziada.
Hata hivyo upigaji kura huo unaendelea licha ya kuwepo kwa kitisho wakati wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo kwani kila chama kinajigamba kuwa kitaibuka na ushindi wa kishindo.
Katika mitaa ya jiji la Tanga uchaguzi unaendelea vizuri mbali ya uchache wa watu wanaojitokeza kupiga kura na makarani wa usimamizi wa uchaguzi baadhi ya vituo  kuchapa usingizi kwa baadhi ya nyakati.
Usipitwe na jambo lolote na niko tayari kukupa kile kinachijiri muda wowote kupitia, kumekuchablog


No comments:

Post a Comment