Ugomvi wa kofia ulienda mbali zaidi, mkasi ukatumika kuyakatisha maisha ya mtu …
Ugomvi wao ulianza kama utani, mmoja
hakupendezwa na utani huo, hata alipokasirika menzake alidhani utani
unaendelea, Agwugho akajikuta akifanya maamuzi ambao yalipelekea rafiki
yake kufariki.
Polisi wa Lagos, Nigeria wamesema wamemkamata mtuhumiwa Joseph Agwugho kwa tuhuma za kumuua rafiki yake Enya Okpara, kwa kumchoma na mkasi, uchunguzi unaonyesha Agwugho na Okpara walikuwa wakigombania kofia ndipo mtuhumiwa alipochukua mkasi na kumchoma nao marehemu shingoni mara tatu.
Okpara alikimbizwa katika Hospitali
Lagos na muda mfupi baadaye kufariki, Agwugho anakabiliwa na kesi ya
mauaji, alipandishwa Kizimbani na baadaye kurudishwa gerezani.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia kumekucha blog
No comments:
Post a Comment