Friday, December 5, 2014

Ukishangaa ya Mussa utacheka ya Firauni



Mzee wa Miaka 85 ahofia kaburi lake kuuzwa na mtoto wake
Cuba2-1231
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mzee mwenye umri wa miaka 80, ameomba msaada wa Serikali kuingilia kati kuzuia shamba lake lisiuzwe na mtoto wake ambapo shamba ambalo mtoto huyo analiuza lina kaburi lake alilolchimba zaidi ya miaka 35 iliyopita.
Shamba la mzee huyo liko Mathira, Kenya ambapo mzee huyo amesema kuwa mtoto wake wa kiume amekuwa akiuza sehemu ya shamba hilo kidogo kidogo.
Amesema tofauti na matarajio yake alikuwa akiamini Mtoto huyo angekuja kumsaidia uzeeni lakini mtoto huyo, amekuwa akiuza shamba hilo bila ruhusa yake na kuhofia kuwa anaweza kuuza hata kipande cha Shamba ambacho amechijimbia kaburi lake.

No comments:

Post a Comment