Kumekucha blog
Tanga,JAMII ya walemavu Mkoa wa Tanga
wameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo Ustadi (Veta) kujenga chuo kikuu maalumu kwa walemavu ili kutoa hamasa kwao
katika kusoma na kujiendeleza kimasomo
shuleni.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kongamano la walemavu wa
viungo na wasiona jana, Mratibu wa Walemavu Wasiona Tanga (TLB), Jumaa
Mwakachalika, alisema kuwepo kwa chuo hicho itakuwa chachu kwa jamii ya
walemavu kielimu.
Alisema changamoto hiyo pia itawasukuma wazazi wenye watoto
walemavu kuwabidiisha watoto katika elimu kwa kuelewa kuwa ataweza kusoma masomo
ya juu Chuo Kikuu baada ya kuwepo kwa misingi ya kumfikisha huko.
“Kama walemavu watajengewa chuo kikuu maalumu kwa ajili yao
ni wazi kabisa wazazi na watoto wenyewe watakuwa na misukumo ya kujibidiisha
darasani----na hii ni kutambua kuwa iko siku atasoma chuo kikuu” alisema
Mwakachalika
“Hii sio kuwa ni ubaguzi bali tutaka kuongeza changamoto
katika ushindani wa kielimu nchini---kuna dhana kuwa walemavu hawawezi kufika
masomo ya juu kama walivyo wengine jambo ambalo tunataka kufuta msemo huo”
alisema
Kwa upande wake mlemavu wa viungo, Mwanahawa Tuwa, ameitaka
Serikali kuwalazimisha wajenzi wa majengo ya huduma za umma kukumbuka kuweka
miundombinu ya walemavu.
Alisema majengo mengi yahana miundombinu hiyo na badala yake
wamekuwa wakijenga njia ya kupita kwa gorofa ya kwanza chini na hivyo kushindwa
kuzifikia huduma nyengine majengo yenye
zaidi ya gorofa moja.
“Majengo mengi hayana miundombinu ya walemavu na hata yale
ambayo yako nayo wamejenga sehemu ndogo tu ya kuingia katika jengo-----zaidi ya
hapo huna ofisi nyengine ambayo unaweza kufika” alisema Tuwa
Alisema hali hiyo imekuwa ikiwasababishia walemavu wengi
kushindwa kupata huduma kwa wakati na usahihi baada ya baadhi ya mambo
kutumishia hata jambo ambalo ni siri.
Alishauri Serikali kuzuia vibali vya ujenzi kwa wakandarasi
ambao hawana michoro ya miundombinu ya walemavu ikiwa na pamoja kuweka sheria ujenzi wa majengo ya Serikali na umma.
Mwisho
No comments:
Post a Comment