Sunday, December 14, 2014

WANAFUNZI WADAI PUNGUZO NAULI ZA MABASI,MIKOANI



Kumekucha blog
Tanga,WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari Tanga, wameitaka Serikali kuweka utaratibu maalumu wa nauli za mabasi kama ilivyo kwa daladala ili kuwa msaada  vipindi vya mwisho wa mwaka kujumuka na  familia zao katika sherehe mbalimbali zikiwemo za sikukuu za Krismass.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kituo kikuu cha mabasi yaendayo Mikoani cha Kange, walisema wanashindwa kusafiri kujumuka na familia zao kutoka na gharama kubwa za nauli za mabasi.
Walisema hiyo inatokana na baadhi ya familia kuwa na uwezo mdogo wa kutuma nauli na hivyo kukosa nafasi kuungana katika mambo mbalimbali muhimu kama misiba na sherehe za sikukuu ya Krismass na Idd kwa Waislamu.
“Hapa sisi tunaelekea Mwanza na nauli iko elfu sitini utadhani ni ya ndege---wazazi wetu ni masikini hawana uwezo wa nauli ya kwenda na kurudi na ndio mara nyingi likizo huwa tunajikalia shule” alisema Gosper Mwalilino
“Kama Serikali ingeweka utaratibu wa nauli kwa wanafunzi kama ilivyo kwa daladala ingekuwa msaada sana----hali hii inawaumiza wazazi wetu na sisi wenyewe hasa sie tunaokaa mbali” alisema
Alisema vipindi vya likizo kubwa mashuleni wanafunzi wamekuwa wahanga wakubwa wa nauli za mabasi na hivyo kuitaka Serikali kuliangalia kwa upande wao wa wanafunzi.
Kwa upande wake mwanafunzi  shule ya Gallanosi , Vicky Kimario,anaetokea Arusha alisema mara nyingi vipindi vya likizo hujikalia shuleni baada ya kushindwa kumudu gharama za nauli za mabasi.
Alisema hali hiyo inakuja baada ya nauli kupanda maradufu na hivyo kuwa katika mazingira magumu ya kuweza kuishi shuleni hapo baada ya huduma zote muhimu kusitishwa ikiwemo ya upatikanaji wa chakula.
“Mwaka jana sikuweza kwenda nyumbani kwani nilishindwa kutokana na nauli kupanda maradufu---na mwaka huu naona yametokea yele yale na baba amenitumia elfu ishirini na ukitoa kuna makato ambayo sitioweza kukata tikiti” alisema Kimario
Ameitaka Serikali kuwawekea utaratibu wa nauli kwa wamiliki wa mabasi yaendayo Mikoani wanafunzi vipindi vya likizo na kuweza kujumuika na familia zao katika vipindi vya sikukuu.
                                                  Mwisho

No comments:

Post a Comment