Tuesday, December 16, 2014

WEZI WA NYAYA ZA UMEME WAKATA NGUZO TATU KWA KUTUMIA MSUMENO WA CHENSOO



KUMEKUCHA BLOG
Korogwe,WATU kumi wanaosadikika kuwa wezi wamekata nguzo tatu za umeme kwa kutumia msumeno aina ya Chensoo kisha kuiba nyaya za umeme aina ya kopa kijiji cha Magoma Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Tukio hilo lilitokea jana saa 8 usiku baada ya wakazi kijiji cha magoma kusikia kishindo kikubwa kilichoambatana na kukatika umeme na hivyo kuingiwa na hofu jambo ambalo liliwasukuma kuamshana na kwenda uelekeo wa mshindo huo.
Wakizungumza katika eneo la tukio, wakazi hao walisema baada ya kishindo hicho waliamshana kwa kuamini kuwa kuna kitendo cha kihalifu na hivyo kupiga simu kituo cha polisi Korogwe na wao  kuzifuatiliza nguzo za umeme moja baada ya moja.
“Kilipiga kishindo kikubwa kilichoambatana na kukatika umeme kitu ambacho si cha kawaida kwetu----tuliamshana kwa kutumia simu na  tukakutana kwa kiongozi wetu wa Serikali” alisema Mohammed Nassour Bodo
“Tuliamini kuwa kishindo kilichoambatana na kukatika umeme ni hujuma imefanyika na hivyo kuzifuatilia nguzo moja baada ya nyengine----tulipofika katika shamba la mahindi tulisikia sauti za watu wazungumza kwa kutoa vitisho” alisema Bodo
Bodo alisema wakati wamefika katika nguzo ambazo zimeangushwa hawakuona nyaza za umeme kitendo ambacho kinamaanisha wezi hao walishazikata na kutoweka nazo.
Wakati maofisa wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa na Wilayani wakiongozwa na Meneja wake wa Korogwe, Bakary Suleiman, aliendesha msako katika vijiji vya jirani kwa lengo za kuzitafuta nyaya hizo kwa kuamini kuwa bado hazijatoweka kijijini hapo.
Wakati za zoezi hilo pia likiwashirikisha maofisa usalama wa Wilaya walifanikiwa kuzikuta roli mbili zikiwa zimefichwa katika pori jirani eneo la tukio.
“Tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea katika Wilaya yangu----kwa kweli kwanza niwashukuru wakazi wa kijiji cha Magoma kwa ushirikiano wao na umoja waliouonyesha kwa Tanesco” alisema Suleiman
Aliwataka kuwa na umoja na mshikamano katika mambo mbalimbali yakiwemo ya kimaendeleo pamoja na kuwa na ada ya kutoa taarifa za kihalifu kama ambavyo wamefanya kwa shirika hilo.
Wakati wa zoezi hilo la kuwatafuta wezi waliofanya hujuma hizo, Afisa Uhusiano na Wateja Mkoa wa Tanga, Monica Mabada, amezitaka mamlaka za Serikali za vijijini na vitongoji kuunda vikosi askari jamii lengo likiwa ni kuyaweka maeneo yao kuiusalama.
Alisema kuwepo kwa askari jamii katika maeneo yao kunaweza kuwa msaada wa usalama wao pamoja na mali zao na hivyo kuwataka kulitekeleza jambo hilo ambalo litaepusha vitendo vya kihalifu nahujuma.
                                                 Mwisho


No comments:

Post a Comment