Monday, December 15, 2014

KHAMISI TAMBWE ATUA YANGA

Kama unalifatilia soka la bongo basi hii mpya kuhusu usajili uliofanywa na Yanga isikupite.


Kama unalifatilia soka la bongo basi hii mpya kuhusu usajili uliofanywa na Yanga isikupite.

DSC07113Taarifa zilizoingia kwenye mtandao huu dakika chache zilizopita ni kwamba Dar es Salaam Young Africans imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Khamisi Tambwe ambapo anaingia kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Hamis Kiiza ambaye amejiunga na URA ya Uganda.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha na kocha Patrick Phiri.
Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya Kenya ambapo sasa Yanga imekamilisha usajili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa kama ilivyopangwa na TFF.
Tambwe 1Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog

No comments:

Post a Comment