Hekaheka ya leo Desemba15 iko hapa, inahusu Mtoto aliyedondoka juu ya friji na kufariki.
Baba wa mtoto huyo amesema alipata
taarifa za kuumia kwa mtoto wake na alipofika Hospitali alikuta hali ya
Mtoto ikiwa mbaya na akilia sana kwa maumivu, baada ya kupatiwa matibabu
waliruhusiwa na kurudi nyumbani.
Siku iliyofuata mtoto alizidiwa na kesho
yake wakamrudisha tena Hospitali ya Amana, baada ya uchunguzi
kufanyika ilionekana Mtoto aliumia sehemu ya kichwani na kushauriwa
kumhamishia Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi na kabla
yakupatiwa matibabu akafariki.
Mwili wa Mtoto huyo umehifadhiwa katika
Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi na Babu ambaye
oinasemekana amehusika kuanguka kwa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la
Polisi.
No comments:
Post a Comment