Sunday, December 14, 2014

MTOTO ASAGWASAGWA NA MASHINE YA KUFULIA

Kilichomkuta baba baada ya mwanaye wa miaka minne kuingia kwenye mashine ya kufulia


http://www.dreamstime.com/royalty-free-stock-photo-laundry-image8649325Baba mmoja nchini Marekani amefungwa jela kwa kosa la kuua baada ya mtoto wake wa miaka minne kuingia ndani ya mashine ya kufulia.
Chanzo cha taarifa hii kimeeleza kuwa baba huyo mwenye miaka 28 aliyetambulika kwa jina la Joseph Blocker mwenye watoto wawili alikua akiwatunza watoto wake vizuri lakini alijikuta akikabiliwa na kosa hilo la uzembe.
Baada ya kuwasili askari hao walikuta mtoto wake wa kiume mweye miaka minne aliyefahamika kwa jina la Koda amefariki dunia baada ya kufungiwa katika mashine hiyo ya kufulia wakati ikifanya kazi.
dad
Chanzo hicho kilidai haikufahamika mara moja kama mtoto huyo aliamua kupanda na kuingia mwenyewe ndani ya mashine hiyo ama kulazimishwa na mtu.
Lakini baadaye iligundulika baba yake alihusika na mauaji hayo baada ya kuwepo pekee ndani wakati tukio la mtoto huyo kuingia ndani ya mashine likifanyika.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, kumekucha blog

No comments:

Post a Comment