255 ya leo December 18 iko hapa, Dr. Dre, Ray C ni baadhi ya waliosikika kwenye hii ya leo
Rapper na mfanyabiashara Dr. Dre
ametoa zawadi kibao pamoja na fungu la kama dola 10,000 kwa kila mtu
ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ambayo inasimamia masuala yake ya
Kisheria kama bonus kwa kazi yao nzuri 2014.
Msanii Ray C
amesema ameahirisha kutoa wimbo wake mpya siku ya leo kutokana na
kutokea kwa msiba wa aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha
Madinda.
Ray C amesema anatarajia kuuachia wimbo huo ndani ya wiki ijayo japo kwa sasa tayari unapatikana kwenye mitandao.
Mazishi ya Aisha Madinda
iliyokuwa yafanyike leo yameahirishwa kutokana na mwili wake kuendelea
kufanyiwa uchunguzi Hospitali na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho
baada ya uchunguzi huo kukamilika.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia
mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia kumekucha blog
No comments:
Post a Comment