Tuesday, December 16, 2014

WEZI WAKATA NGUZO TATU ZA UMEME KWA KUTUMIA MSUMENO WA CHEINSOO


 Meneja Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Wilaya ya Korogwe, Bakary Suleiman akiwaonyesha waandishi wa habari moja katika ya nguzo tatu zilizokatwa na wezi wa nyaya za umeme waliotumia msumeno aina ya Chensoo kijiji cha Magoma Wilayani humo juzi usiku.


  Afisa usalama wa polisi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga akiwaonyesha waandishi wa habari shati lililoachwa na mmoja wa wezi wa nyaya za umeme waliokata nguzo tatu kwa kutumia msumeno aina ya Chensoo juzi usiku.


 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Bakary Suleiman kushoto pamoja na wakazi wa kijiji cha Magoma Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakiangalia hujuma zilizofanywa na wezi kwa kukata nguzo tatu za umeme saa 8 usiku kutumia msumeno aina ya Chensoo kisha kuiba nyaya  na kutokomea.
  Afisa Uhusiano Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Tanga, Monica Mabada, kulia pamoja na Afisa Usalama upelelezi Wilaya ya Korogwe Markyagadi Makumba wakiangalia moja ya nguzo tatu zilizokatwa na wezi wa nyaya za umeme kijiji cha Magoma Wilayani humo tukio lililofanywa saa 8 usiku juzi.

No comments:

Post a Comment