Tuesday, April 21, 2015

MOHAMMED MORSI JELA MIKA 20

Mahakama ya Misri imeamua adhabu hii kwa Rais wao wa zamani!!

mosi
Makahama ya Misri  imetoa hukumu kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi  kutokana na kuuawa kwa waandamanaji wengi wakati akiwa madarakani.
Hukumu hiyo iliolewa leo kwa Rais huyo tangu aondoke madarakani mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake sasa amehukumiwa jela miaka 20.
Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa vurugu nje ya Ikulu ya nchi hiyo mwishoni mwa mwaka 2012.
Wakati umati ulipokusanyika nje ya Ikulu  Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.
mahakamanBaadaye Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa kwenye vurugu hizo, wengi kutoka kundi la Muslim Brotherhood.
Kabla ya kutolewa hukumu  leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukusogezea muda wote kupitia hapa hapa www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment