Unaambiwa hii treni nd’o imevunja rekodi ya kwenda kasi zaidi DUNIANI..
Wasafiri wote wanapenda usafiri wa
haraka, salama na wa uhakika.. sasa inapokuja kwenye teknolojia wenu
wametuacha mbali kiukweli.. Kwa TZ ukitaka kusafiri haraka kwenda zako Mwanza au Mbeya inabidi tu upande zako Fast Jet ili uwahi.
Niliwahi kusikia story za watu wanasimuliana eti mtu anakaa umbali kama wa Dar-Moro, anaishi Morogoro anafanya kazi Dar..
na kila siku anawahi kazini, usafiri unaotegemewa zaidi ni treni za
umeme. Japan wanaingia kwenye HEADLINES za maendeleo mengine kwenye
Teknolojia, wametengeneza treni ambayo inasafiri kumbali wa Kilometa
603 kwa saa moja.. hesabu ya kwanza nikawaza kama ni safari ya Mbeya inachukua saa 1 na nusu, kwa sababu Dar-Mbeya ni Kilometa kama 840 hivi.
Mwanza je? Dar-Mwanza ni kama kilometa 1,150.. hiyo safari inakamilika ndani ya saa mbili tu !!
Japan wana mpango wa treni hiyo kuanza kazi kati ya miji ya Tokyo na Nagoya mwaka 2027, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe atakuwa Marekani ndani ya wiki hii kuangalia jinsi watakavyoweza kujenga reli kwa ajili ya treni hiyo kati ya New York na Washington D.C.
Kingine cha kukufikishia ni kwamba
tumezoea kuona treni zenye tyre za chuma ambazo zinatembea kwenye reli,
hii inatumia sumaku ambazo zinatumia umeme.
No comments:
Post a Comment