Umeisikia hii ya mwanamke kuolewa mara mbili? Mume wa pili hata hakujua..
Ishu
ni kwamba kuna mwanaume alikutana na msichana wakapeana namba za simu
wakawa wanawasiliana, wakaanzisha uhusiano, baadae wakafunga ndoa..
kilichoibuka baadae kumbe yule mwanamke ni mke wa mtu !!
Mwanaume huyo amesema alipokutana na
mwanamke huyo alimwambia kuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu,
wakaendelea na uhusiano hadi binti alipomueleza kuwa amemaliza shule na
kujiunga VETA, akasoma mpaka akamaliza. uhusiano wao ulidumu kwa miaka
miwili, hakuna tatizo lolote lilitokea hapo katikati.
Wakakubaliana waoane.. Mwanaume akapeleka barua ya posa kwa wazazi wake na harusi ikafungwa nyumbani kwao Zanzibar.
Wakiwa ukumbini wazazi wa mwanaume
wakasikia tetesi kuwa mwanamke huyo ameolewa na ana familia yake..
wakaanza kufuatilia na kugundua kuwa mwanamke huyo ameolewa na ana
watoto wanne, yuko kwenye ndoa kwa miaka 16.. ndoa hii mpya haikwenda
mbali, ilivunjika ndani ya wiki moja.
No comments:
Post a Comment